Friday, July 6, 2012

AZAM YASHINDA 3-2 ZANZIBAR

Na Somoe Ng'itu, Zanzibar
TIMU ya soka ya Azam FC imepata ushindi wake wa kwanza katika mechi tatu za kwanza za Kombe la Urafiki baada ya kuilaza Mafunzo ya hapa kwa mabao 3-2 katika mechi iliyojaa ushindani kwenye Uwanja wa Amaan hapa Zanzibar.

Azam walianza mechi hiyo vizuri na kuongoza kwa magoli 2-0 kupitia kwa Ramadhani Chombo "Redondo" ambaye alitupia la kwanza mapema katika kipindi cha kwanza kabla ya Kipre Tchetche kuongeza la pili katika dakika ya 34 na hivyo kwenda mapumziko wakiongoza kwa kujiamini.

Hata hivyo, dakika ya kwanza baada ya mapumziko, wenyeji walipata bao la kwanza kupitia kwa Sadick na wakaongeza la pili katika dakika ya 62 kupitia kwa Mohammed Abdulrahman na kufanya ngoma kuwa 2-2.

Zikiwa zimesalia dakika 8 mchezo kumalizika, Ibrahim Mwaipopo aliifungia Azam bao 3 lililoifanya Azam kufikisha pointi tano baada ya mechi tatu.

Katika mechi ya kwanza, Azam walitoka sare ya 1-1 dhidi ya Karume Boys (U23) ya Zanzibar kabla ya kutoka sare nyingine ya 1-1 dhidi ya Simba.

Mabingwa wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara, Simba watacheza mechi yao ya tatu wakati watakapowavaa Karume Boys (U23) ya Zanzibar baadaye leo.

Katika mechi ya kwanza Simba waliibwaga Mafunzo kwa mabao 2-0 kabla ya kutoka sare ya 1-1 na Azam. Simba wana pointi nne na mechi moja mkononi nyuma ya Azam
.

Azam yapiga la tatu. Ni 3-2. LIVE KUTOKA Z'BAR

SOMOE NG'ITU ANARIPOTI LIVE KUTOKA ZANZIBAR

Dk. 82. Ni 3-2. Azam yazinduka. Ibrahim Mwaipopo ameifungia Azam bao 3 dhidi ya Mafunzo.

Mafunzo waliotanguliwa kwa 2-0 walisawazisha yote mawili kupitia kwa Sadick na Mohammed Abdulrahman na kufanya ngoma kuwa 2-2 katika mechi yao ya tatu ya Kombe la Urafiki.

Ramadhani Chombo "Redondo"  alitupia la kwanza mapema kipindi cha kwanza na Kipre Tchetche akaongeza la pili katika dakika ya 34.

Katika mechi ya kwanza, Azam walitoka sare ya 1-1 dhidi ya Karume Boys (U23) ya Zanzibar kabkla ya kutoka sare ya 1-1 tena dhidi ya Simba.

Mabingwa wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara, Simba leo watacheza mechi ya pili usiku dhidi ya Karume Boys (U23) ya Zanzibar.

Katika mechi ya kwanza Simba waliibwaga Mafunzo kwa mabao 2-0 kabla ya kutoka sare ya 1-1 na Azam.

Azam hoi sasa ni 2-2: LIVE KUTOKA Z'BAR

SOMOE NG'ITU ANARIPOTI LIVE KUTOKA ZANZIBAR

ZANZIBAR dk 62. Azam hoi. Mafunzo wamesawazisha zote mbili kupitia kwa Sadick na Mohammed Abdulrahman. Ngoma sasa ni 2-2 katika mechi yao ya Kombe la Urafiki.

Ramadhani Chombo "Redondo"  alitupia la kwanza mapema kipindi cha kwanza na Kipre Tchetche akaongeza la pili katika dakika ya 34.

Katika mechi ya kwanza, Azam walitoka sare ya 1-1 dhidi ya Karume Boys (U23) ya Zanzibar kabkla ya kutoka sare ya 1-1 tena dhidi ya Simba.

Mabingwa wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara, Simba leo watacheza mechi ya pili usiku dhidi ya Karume Boys (U23) ya Zanzibar.

Katika mechi ya kwanza Simba waliibwaga Mafunzo kwa mabao 2-0 kabla ya kutoka sare ya 1-1 na Azam.

AZAM YAONGOZA 2-0: LIVE KUTOKA ZANZIBAR

Ramadhani Chombo 'Redondo' mfungaji wa bao la kwanza la Azam katika mechi ianyoendelea kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar

SOMOE NG'ITU ANARIPOTI LIVE KUTOKA ZANZIBAR

ZANZIBAR kipindi cha pili kinaanza. Azam wanaongoza 2-0 dhidi ya Mafunzo katika mechi yao ya Kombe la Urafiki.

Ramadhani Chombo "Redondo"  alitupia la kwanza mapema kipindi cha kwanza na Kipre Tchetche akaongeza la pili katika dakika ya 34.


Katika mechi ya kwanza, Azam walitoka sare ya 1-1 dhidi ya Karume Boys (U23) ya Zanzibar kabkla ya kutoka sare ya 1-1 tena dhidi ya Simba.
 
Mabingwa wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara, Simba leo watacheza mechi ya pili usiku dhidi ya Karume Boys (U23) ya Zanzibar.

Katika mechi ya kwanza Simba waliibwaga Mafunzo kwa mabao 2-0 kabla ya kutoka sare ya 1-1 na Azam. 

ANGALIA UTAMBULISHO WA JORDI ALBA BARCELONA

Jordi Alba akipozi kwa picha baada ya kusaini mkataba wa kujiunga na FC Barcelona kwenye Uwanja wa Camp Nou Julai 4, 2012 mjini Barcelona, Hispania.

Jordi Alba akisaini kumbukumbu za mashabiki huku akizungukwa na wana habari baada ya kusaini mkataba wa kujiunga na FC Barcelona kwenye Uwanja wa Camp Nou juzi (Julai 4, 2012) mjini Barcelona, Hispania.
Jordi Alba akiingia uwanjani kwa ajili ya kutambulishwa rasmi kama mchezaji wa FC Barcelona kwenye Uwanja wa Camp Nou jana (Julai 5, 2012) mjini Barcelona, Hispania.
Jordi Alba akipungia mashabiki wakati wa kutambulishwa rasmi kama mchezaji wa FC Barcelona kwenye Uwanja wa Camp Nou jana (Julai 5, 2012) mjini Barcelona, Hispania.
Jordi Alba akibusu nembo ya Barcelona wakati wa kutambulishwa rasmi kama mchezaji wa FC Barcelona kwenye Uwanja wa Camp Nou jana (Julai 5, 2012) mjini Barcelona, Hispania.
Jordi Alba akipozi uwanjani wakati wa kutambulishwa rasmi kama mchezaji wa FC Barcelona kwenye Uwanja wa Camp Nou jana (Julai 5, 2012) mjini Barcelona, Hispania.


Hebu soma jina lake linavyosomeka mgongoni....

Mambo haya waulize akina Balotelli........

Mambo yatakuwa DOLE tu msimu huu.... yani shavu la huku mimi, la kule Dani Alves. Nomaaaaa!

ODHIAMBO WA AZAM APATA ITC


SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limepokea Hati ya Uhamisho wa Kimataifa (ITC) ya mchezaji George Odhiambo, raia wa Kenya aliyejiunga na klabu ya Azam.

Hati hiyo imetolewa na Chama cha Mpira wa Miguu cha Denmark (DBU) ambapo Odhiambo alikuwa akicheza nchini humo kabla ya kutua Azam kwa ajili ya msimu wa 2012/2013.

Klabu nyingine zinazosajili wachezaji kutoka nje ya Tanzania zinatakiwa kuhakikisha zinakamilisha uhamisho wao (transfer) kabla ya Julai 30 mwaka huu ambayo ndiyo siku ya mwisho kufanya hivyo.

Kanuni ya 41 ya Ligi Kuu kuhusu ITC inasema: “(1) Maombi ya ITC kwa wachezaji wa kigeni wa kulipwa yatawasilishwa kupitia mtandao wa kompyuta kwa kutumia program ya ‘Transfer Matching System-TMS’ baada ya klabu zinazohusika na mchezaji huyo au wachezaji hao kukubaliana nje ya mtandao.

(2) Maombi ya ITC kwa wachezaji wa kigeni wasio wa kulipwa yatawasilishwa kwa barua TFF baada ya klabu zinazohusika na mchezaji huyo au wachezaji hao kukubaliana. Chama cha Soka kinachotoa ITC kwa njia hii kitapeleka nakala FIFA. (3) ITC haihitajiki kwa mchezaji mwenye umri chini ya miaka kumi na mbili (12).”

Tunapenda kuzikumbusha klabu kuwa kwa mujibu wa Kanuni ya 53 ya Ligi Kuu, wachezaji wa kigeni ni lazima wawe wanachezea timu ya Taifa au klabu za Ligi Kuu huko wanakotoka.

Kanuni hiyo inasema: “Klabu inaruhusiwa kusajili wachezaji wa kigeni wa ngazi ya kimataifa ambao ni wa timu za Taifa na Ligi Kuu kutoka nje ya nchi wasiozidi watano (5). Wachezaji kutoka Ulaya na Marekani ya Kusini wanweza kuwa wa daraja la pili na kuendelea, na klabu inaruhusiwa kuchezesha wachezaji walioorodheshwa wasiozidi watano (5) wa kigeni katika mchezo mmoja. Wachezaji hao watasajiliwa baada ya TFF kuhakikisha usahihi wa taarifa zao na kukamilika kwa taratibu za uhamisho wa kimataifa.”

SABA WAPATA ITC KUCHEZA KENYA, MSUMBIJI

SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetoa Hati ya Uhamisho wa Kimataifa (ITC) kwa Watanzania saba kucheza mpira wa miguu katika nchi za Kenya na Msumbiji.

TFF imetoa hati hizo kwa wachezaji hao baada ya kuombewa na Shirikisho la Mpira wa Miguu la Kenya (FKF) na Shirikisho la Mpira wa Miguu la Msumbiji (FMF) ili waweze kucheza katika klabu za nchi hizo.

Wachezaji waliokwenda Bandari ya Kenya na klabu walizokuwa wakichezea nchini kwenye mabano ni David Naftali (huru), Meshack Abel (huru), Mohamed Banka (huru) na Thomas Mourice (Mtibwa Sugar).

Klabu ya CD Madchegde ya Msumbiji imewachukua wachezaji Hassan Hassan Mustapha kutoka Mgambo Shooting ya Tanga, na Abdallah Ally Abdallah na Thobias David Silas kutoka klabu ya daraja la kwanza ya Transit Camp ya Dar es Salaam.

16 BORA COPA COCA-COLA KUANZA J’MOSI

16 bora ya michuano ya Copa Coca-Cola 2012 inaanza kesho (Julai 7 mwaka huu) kwa mechi nne zitakazokutanisha timu nane kati ya 16 zilizofuzu hatua hiyo. Mechi hizo za 16 bora zitachezwa kwenye viwanja vya Kumbukumbu ya Karume na Tanganyika Packers vya Dar es Salaam.

Ruvuma iliyoongoza kundi A itacheza na Temeke iliyoshika nafasi ya tatu kundi C. Mechi hiyo itaanza saa 2.30 asubuhi Uwanja wa Karume. Mechi nyingine ya asubuhi itakayochezwa Tanganyika Packers itawakutanisha washindi wa pili kundi A Kigoma dhidi ya Mara walioshika nafasi ya nne kundi C.

Mechi za jioni kwa kesho zitakazoanza saa 10 kamili jioni zitakuwa kati ya Mjini Magharibi na Kagera kwenye Uwanja wa Karume wakati Morogoro na Pwani zitaumana kwenye Uwanja wa Tanganyika Packers ulioko Kawe, Dar es Salaam.

Hatua ya 16 bora itakamilika keshokutwa (Julai 8 mwaka huu) kwa mechi za asubuhi kati ya Kinondoni na Rukwa kwenye Uwanja wa Karume, na Dodoma dhidi ya Arusha kwenye Uwanja wa Tanganyika Packers. Mechi za jioni siku hiyo ni kati ya Kilimanjaro na Mwanza (Uwanja wa Karume) na Tabora na Tanga (Tanganyika Packers).

Timu zitakazoshinda zitaingia hatua ya robo fainali itakayochezwa Julai 10 na 11 mwaka huu kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume. Nusu fainali itachezwa Julai 13 mwaka huu, na kufuatiwa na mechi ya mshindi wa watatu na fainali ambazo zote zitachezwa Julai 15 mwaka huu.

UNAJUA TEKNOLOJIA YA GOLI INAVYOFANYA KAZI? SOMA HAPA

*Ligi Kuu ya England kuanza kuitumia msimu huu 2012-13

John Terry wa England akiosha wavuni goli la Ukraine ambalo halikuhesabiwa wakati wa mechi yao ya hatua ya makundi ya Euro 2012. Ukraine walilala 1-0.

 

ZURICH, Uswisi
TEKNOLOJIA ya mstari wa goli huenda ikaanza kutumika kwenye Ligi Kuu ya England katikati ya msimu huu wa 2012-13 baada ya Bodi ya Kimataifa ya Kusimamia Mchezo wa Soka (IFAB) kuidhinisha matumizi ya teknolojia viwanjani mjini Zurich.

Aina mbili za teknolojia - Jicho la Mwewe (Hawk-Eye) na Refa wa Lango (GoalRef) - zimepitishwa na FIFA kutumika.

Teknolojia inatumika kwa mara ya kwanza kwenye fainali za Kombe la Dunia la Klabu la FIFA Desemba na, kama itaonyesha mafanikio, itatumika katika Kombe la Shirikisho 2013 na Kombe la Dunia 2014. 

Ligi Kuu ya England imesema inataka kuanza kutumia teknlojia "haraka iwezekanavyo."

Taarifa ya Ligi Kuu ya England kufuatia ruhusa hiyo ya IFAB imesema: "Ligi Kuu ya England imekuwa ikiitaka teknolojia ya goli la mstari kwa muda mrefu.

Katibu Mkuu wa chama cha soka cha England (FA), Alex Horne amesema: "Tunayakaribisha maamuzi haya yaliyotolewa leo na IFAB na tunaingia katika mijadala ya kuamua kutumia teknolojia zote Jicho la Mwewe (Hawk-Eye) na Refa wa Goli (GoalRef) hivi karibuni ili tuanze kuitumia haraka iwezekanavyo."

Horne alisema FA itaamua muda wa kuanza kutumia teknolojia.
"Inaweza kuwa ni Desemba wakati teknolojia itakapokuwa imeshathibitishwa rasmi na kusimikwa," alisema katika mkutano na waandishi wa habari mjini Zurich. "Kipaumbele ni kuanza kutimika katika Kombe la Dunia la FIFA nchini Japan.

"Ligi Kuu ya England inahitaji kuzungumza na kampuni mbili zilizopewa haki za kusambaza teknlojia hiyo na klabu za ligi. Kwa ninachofahamu ni kwamba klabu zinasapoti, na kwa maana hiyo, kama klabu zote zitakubali itaanza kutumika katikati ya msimu, au kabla ya kuanza kwa msimu wa 2013-14."

Dhamira ya kutaka kuleta teknolojia ya goli iliongezeka baada ya Ukraine kunyuimwa goli lao halali la kusawazisha baada ya mpira kuvuka mstari wa lango katika mechi waliyolala 1-0 dhidi ya England katika fainali za Euro 2012.

Kocha wa Chelsea, Roberto Di Matteo amesema: "Tunashuhudia kila msimu, kila kwenye michuano mikubwa, tunahitaji teknlojia hii kwa sababu kuna matukio muhimu mno wakati wa mechi hizo ambapo unaweza kupata suluhisho sahihi kwa kutumia teknolojia."

Rais wa UEFA, Michel Platini anaaminika kwamba anapenda zaidi kutumia waamuzi watano, jambo ambalo limeidhinishwa na FIFA jana.

Mfumo huo, ambao unawashuhudia mwamuzi wa ziada akisimama kwenye kila mstari wa goli na kuzunguka eneo la penalti, umekuwa katika majaribio tangu mwaka 2008 na ulitumika pia wakati wa Euro 2012 pamoja na Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya.

FIFA pia imeondoa katazo wanawake kucheza soka wakiwa wamevaa hijab, jambo linaloruhusu mataifa yenye imani ya dini ya Kiislamu kushiriki michuano mikubwa.




JICHO LA MWEWE LINAFANYAJE KAZI?

Teknolojia ya Jicho la Ndege Tai (Hawk-Eye) inatumia kamera sita, zinazoelekea kwenye kila lango, kuufuatilia mpira uwanjani.

Mfumo huo unatumia kitu kinaitwa "pembetatu" kubaini mpira uko mahala gani hasa.

Kama mpira utavuka mstari wa lango, "ishara" itatumwa kwenye saa ya mkononi ya refa kuashiria kuwa goli limetinga.

Kwa matakwa ya FIFA, tukio hilo zima litatumia chini ya sekunde kukamilika.
 
TEKNOLOJIA YA "GOAL REF" INAFANYAJE KAZI? 


Teknolojia ya "GoalRef" inatumia ki-chip kidogo kinachopandikizwa kwenye mpira na inatumia miale ya sumaku langoni.

Mfumu huo utabaini mabadiliko katika miale ya sumaku ndani ama nje ya lango kutambua kama goli limefungwa.

Tukio hilo zima linatumia muda wa chini ya sekunde moja, na majibu yanamwendea refa kwa umeme refa.