Wednesday, November 28, 2012

TAZAMA 'FULL MAPICHA' YA MAZISHI YA SHAROMILIONEA... WAOMBOLEZAJI KADHAA WAZIMIA NA KUKIMBIZIWA HOSPITALI YA WILAYA MUHEZA... SERIKALI YATANGAZA MSAKO MKALI WA NYUMBA KWA NYUMBA KUWASAKA WALIOPORA VITU VYA MAREHEMU SHAROMILIONEA....MZEE MAJUTO AONGOZA WASANII KIBAO KUMZIKA LEO... WAMO KINA JB, RICHIE, CLAUDI, MUHOGO MCHUNGU, MWANA-FA, WEMA SEPETU, JACQUELINE WOLPER, KINGWENDU, MTUNISI, DUDE , VICENT KIGOSI 'RAY'...!

Twende huku mzee...! Msanii wa vichekesho ambaye ni mshirika wa karibu wa marehemu Sharomilionea, King Majuto (kushoto) akiongozwa na muigizaji JB wakati wa shughuli za mazishi ya Sharomilionea leo mchana kijijini kwao Lusanga, Muheza mkoani Tanga.

Jeneza la marehemu Sharomilionea kabla ya kupelekwa makaburini na mwili wa marehemu kuzikwa kijijini kwao Lusanga, Muheza mkoani Tanga leo Novemba 28, 2012.
 
Waombolezaji wakiwa katika ibada ya sala ya jeneza la marehemu Sharomilionea katika kijiji chao cha Lusanga, Muheza mkoani Tanga leo Novemba 28, 2012.
 
Mwili wa marehemu Sharomilionea ukiswaliwa kabla ya kuzikwa leo mchana (Novemba 28, 2012) kijijini kwao Lusanga, Muheza mkoani Tanga.
Baadhi ya waombol;ezaji waliojitokeza kumzika Sharo Milionea kijijini kwao Lusanga, Muheza mkoani Tanga leo Novemba 28, 2012.
 
Baadhi ya waombolezaji wakiwa kwenye mazishi ya Sharomilionea leo Novemba 28, 2012. 
Ni majonzi tupu... baadhi ya waombolezaji katika mazishi ya Sharomilionea leo Novemba 28, 2012.

Baadhi ya wasanii wa filamu wakiwa wenye majonzi tele wakati wa mazishi ya Sharomilionea kijijini kwao Lusanga, Muheza mkoani Tanga leo Novemba 28, 2012.

Mama wa marehemu Sharomilionea (kulia) akilia kwa uchungu wakati wa mazishi ya mwanawe leo Novemba 28, 2012.


Sehemu ya umati wa watu waliohudhuria mazishi ya Sharomilionea katika Kijiji cha Lusanga, Muheza mkoani Tanga leo Novemba 28, 2012.

Sharomilionea (kulia) enzi za uhai wake akiwa jukwaani na King Majuto. 
Msanii wa vichekesho, King Majuto, aliyekuwa mshirika wa karibu wa marehemu Hussein Ramadhani Mkieti "Sharomilionea" ni miongoni mwa wasanii kibao waliojitokeza leo kumzika mwenzao katika makaburi ya famili yao yaliyoko kwenye kitongoji cha Jibandeni, kwenye kijiji cha Lusanga wilaya ya Muheza mkoani Tanga.

Wasanii wengine walioungana na maelfu ya wananchi walioongozwa pia na viongozi mbalimbali wa serikali na wa kisiasa ni Vincent Kigosi 'Ray', Jacob Steven 'JB', Muhogo Mchungu, Wema Sepetu, Jacqueline Wolper, Mwana-FA, Kingwendu, Singo Mtambalike 'Richie', Dude na Claudi.

Viongozi mbalimbali waliohudhuria mazishi hayo yaliyofanyika saa 7:00 mchana ni pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Muheza, Subira Mgalu,  Mbunge wa Jimbo la Muheza, Herbert Mntangi, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Muheza, Amiri Kiroboto na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye ambaye alimwakilisha Rais Kikwete.

Ibada ya mazishi iliongozwa na Sheikh Twaha Juma na baada ya mwili kuwekwa mbele ya uwanja wa nyumba na kuswaliwa, baadhi ya waombolezaji walijikuta wakianguka na kupoteza fahamu kabla ya kukimbiziwa katika Hospitali Teule ya Wilaya ya Muheza.

Akizungumza mbele ya waombolezaji waliofurika kwa wingi katika msiba huo, Mkuu wa Wilaya, Subira Mgalu, aliwapa siku mbili watu walioiba vitu vya marehemu Sharomilionea kuvirejesha mara moja
kabla hatua kali za kisheria hazijachukuliwa dhidi yao.

Mgalu alisema kuwa baada ya kupita siku hizo zilizoanza kuhesabiwa kuanzia leo, polisi watafanya msako wa kila nyumba na kwamba ni lazima 'mijizi' itabainika na kufikishwa mbele ya vyombo vya sheria.

Sharomilionea alifariki dunia saa 3:00 usiku juzi katika kijiji cha Maguzo, wilaya ya Muheza mkoani Tanga wakati akienda kuwasalimia wazazi wake, nyumbani kwao katika Kijiji cha Lusanga wilayani Muheza.

Inaelezwa kuwa baada ya gari alilokuwa akiendesha aina ya Toyota Harrier kupinduka zaidi ya mara tatu na yeye kupoteza maisha papo hapo, watu wasiojulikana waliuvamia mwili wake na kumkomba vitu vyote huku wakimuacha na soksi na nguo ya ndani tu.

.

2 comments:

  1. pole sana familia na mama yaetu mpendwa kwa kumpoteza sharo, hiyo ni kazi ya ALLAH kilichobaki ni kumuombea duah akapumzike kwa amani.

    ReplyDelete