Friday, July 6, 2012

AZAM YASHINDA 3-2 ZANZIBAR

Na Somoe Ng'itu, Zanzibar
TIMU ya soka ya Azam FC imepata ushindi wake wa kwanza katika mechi tatu za kwanza za Kombe la Urafiki baada ya kuilaza Mafunzo ya hapa kwa mabao 3-2 katika mechi iliyojaa ushindani kwenye Uwanja wa Amaan hapa Zanzibar.

Azam walianza mechi hiyo vizuri na kuongoza kwa magoli 2-0 kupitia kwa Ramadhani Chombo "Redondo" ambaye alitupia la kwanza mapema katika kipindi cha kwanza kabla ya Kipre Tchetche kuongeza la pili katika dakika ya 34 na hivyo kwenda mapumziko wakiongoza kwa kujiamini.

Hata hivyo, dakika ya kwanza baada ya mapumziko, wenyeji walipata bao la kwanza kupitia kwa Sadick na wakaongeza la pili katika dakika ya 62 kupitia kwa Mohammed Abdulrahman na kufanya ngoma kuwa 2-2.

Zikiwa zimesalia dakika 8 mchezo kumalizika, Ibrahim Mwaipopo aliifungia Azam bao 3 lililoifanya Azam kufikisha pointi tano baada ya mechi tatu.

Katika mechi ya kwanza, Azam walitoka sare ya 1-1 dhidi ya Karume Boys (U23) ya Zanzibar kabla ya kutoka sare nyingine ya 1-1 dhidi ya Simba.

Mabingwa wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara, Simba watacheza mechi yao ya tatu wakati watakapowavaa Karume Boys (U23) ya Zanzibar baadaye leo.

Katika mechi ya kwanza Simba waliibwaga Mafunzo kwa mabao 2-0 kabla ya kutoka sare ya 1-1 na Azam. Simba wana pointi nne na mechi moja mkononi nyuma ya Azam
.

No comments:

Post a Comment