Wednesday, August 29, 2012

SERENA WILLIAMS KIBOKO... AJIACHIA BICHI NA KICHUPI WEEE...AFU ATINGA KWENYE MICHUANO YA TENIS YA U.S OPEN NA KUONYESHA KIWANGO CHA JUU HUKU AKITAMBA KWA KUSEMA: MIMI ND'O MKALI WA TENIS NA. 1

Hebu nicheki.... Serena Williams akijaichia katika fukwe za Miami Kusini.
Na pozi hili je...? Serena Williams akifaidi maraha ufukweni.
Kwanza tukanywe madafu ... Serena Williams na shosti wake wakiwa bichi.
Na huku je? Mmmh...fumbeni macho please! Serena Williams akiwa bize na raha za ufukweni.
Sijui niondoe kabisa na hivi vinguo? Serena Williams
Fumbeni macho please...! Vibweka vya Serena Williams wakati akiwa kwenye fukwe za Miami Kusini.
Wacha niwatumie meseji wasomaji wa STRAIKA.
Mwili haujengwi kwa matofali ati...! Hapa Serena akipata vimisosi laini vya bichi.
Mwasho? Mambo ya Serena Williams awapo ufukweni.
Mambo..! Serena Williams akiendelea kujaichia ufukweni. 
Mie nshachoka...nasepa! Serena Williams na mashosti zake wakiondoka baada ya kujiachia kwa sana katika fukwe za Miami Kusini.
Hapa sasa ni kazi tu...mambo ya kula bata hukooooo! Serena Williams akishangilia baada ya kumchapa Coco Vandeweghe katika siku ya pili ya michuano ya tenis  inayoendelea ya US Open 2012 kwenye kituo cha tenis cha USTA Billie Jean King jijini New York jana.   
NEW YORK, Marekani
Licha ya kuonekana mwezi huu akijiachia mara kadhaa huku akiwa na "kichupi" tu katika fukwe za kusini mwa Miami, nyota huyo wa tenis ameonyesha kiwango cha juu katika michuano ya tenis ya U.S Open na kushinda kwa pointi 6-1 6-1 dhidi ya Coco Vandeweghe kabla ya kutinga raundi ya pili huku akitamba kuwa yeye ndiye Na.1 duniani kwa sasa na hakuna mkali mwingine zaidi yake.

Kwa mujibu wa viwango rasmi vya mchezo wa tenis kwa upande wa wanawake duniani, Serena Williams anakamata nafasi ya nne, akizidiwa na akina Victoria Azarenka.

"Hilo liko wazi... najichukulia kuwa mimi nd'o namba moja kwa ubora wa tenis duniani," amesema Serena.

"Kuna wachezaji wengi katika mchezo huu... sijali kuhusu nafasi yangu katika viwango vinavyotolewa vya ubora wa tenisi. Nimekuwa namba moja. Niko poa. Lengo langu ni kuwa mchezaji bora duniani. Kama ninashinda na bado siwi namba moja, poa tu."

Baada ya kutinga raundi ya pili ya michuano ya U.S Open   inayoendelea kwenye uwanja wa kituo cha USTA Billie Jean King jijini New York, Serena sasa atacheza dhidi ya Mhispania Maria Jose Martinez Sanchez.

No comments:

Post a Comment