Wednesday, August 15, 2012

NYOKA ALIYEZUA GUMZO KWENYE MITANDAO YA KIJAMII

Muunganiko wa picha za anayedaiwa kuwa nyoka mkubwa aliyeuawa Misri
MTU asiyejulikana amezua mjadala mkubwa kwenye mitandao ya kijamii baada ya ku-post picha ya anayedaiwa kuwa nyoka mkubwa wa aina ya Anaconda, anayedaiwa kuuawa kwenye Bahari ya Shamu baada ya kuua watalii 320 na madereva 125 wa Misri.

Taarifa ya mtu huyo ambayo haijathibitishwa, ilidai kuwa nyoka huyo aliuawa na timu ya wanasayansi wakubwa wa Misri na wapigambizi waliofuzu.

Yakatajwa pia mjina ya wanasayansi waliodaiwa kufanikisha kuuawa kwa nyoka huyo kuwa ni Dk. Karim Mohammed, Dk. Mohammed Sharif, Dk. Mr. Sea, Dk. Mahmoud na Dk. Mazen Al-Rashidi.

Wapigambizi waliotajwa katika kumkamata nyoka huyo mkubwa ni Ahmed ambaye alikuwa kiongozi wa shughuli hiyo, Abdullah Karim, mvuvi Knight, Wael Mohammed, Mohammed Haridi, mpiga mikuki Alvajuma na Mahmoud Shafik, ambaye ni polisi.


Ikadaiwa kuwa mwili wa nyoka huyo umepelekwa katika makumbusho ya kimataifa ya wanyama Misri ya Sharm El Sheikh.


Hata hivyo, mijadala katika mitandao ya kijamii imeshambulia vikali taarifa hiyo ikisema haina ukweli wowote.



1 comment: