Wednesday, November 28, 2012

TAZAMA MAPICHA ZAIDI NAMNA AJALI ILIYOMUUA SHAROMILIONEA ILIVYOHARIBU VIBAYA PIA GARI ALILOKUWA AKIENDESHA... MIJITU YENYE ROHO YA SHETANI YAMKOMBA KILA KITU NA KUUACHA MWILI WAKE UKIWA NA 'BOXER' TU... MBUNGE HERBET MTANGI WA MUHEZA AONGOZA MAELFU YA WATU KWENDA KUSHUHUDIA MWILI WAKE HOSPITALINI... KAMPUNI YA SIMU YA AIRTEL YAMLILIA BAADA YA KUWAPAISHA VIBAYA SANA KWA TANGAZO LAKE KALI LA 'UMEBUGI MEEEN'...!


Gari alilokuwa akiendesha Sharomilionea linavyoonekana katika eneo la ajali.
Baadhi ya wananchi wakilitazama gari alilokuwa akiendesha Sharomilionea na kuharibika vibaya baada ya kupinduka na kumsababaishia umauti.

Wananachi wakiendelea kutazama mabaki ya gari aina ya Toyota Harrier lenye namba za usajili T 478 BVR alilokuwa akiliendesha Sharomilionea kabla halijapinduka na kumsababaishia umauti. 
.
Hapa linavyoonekana gari alilokuwa akiendesha marehemu Sharomilionea linavyoonekana kwa nyuma.Mbunge wa Jimbo la Muheza, Herbet Mtangi (kushoto) akiwa katika Hospitali Teule ya Muheza ulikohifadhiwa mwili wa marehmu Sharomilionea.


Hatuamini... tunataka kuhakikisha! Baadhi ya wananchi wakiwa nje ya chumba cha maiti cha Hospitali Teule ya Wilaya ya Muheza kushuhudia mwili wa marehemu Sharomilionea aliyefariki kwa ajali ya gari. 
Mbunge wa Jimbo la Muheza, Herbet Mtangi ni miongoni mwa maelfu ya watu waliomiminika katika Hospitali Teule ya Wilaya ya Muheza kushuhudia mwili wa msanii wa vichekesho na muimbaji wa muziki wa kizazi kipya, Hussein Mkietty a.k.a Sharomilionea ambaye alifariki kwenye ajali mbaya ya gari juzi usiku huku taarifa zaidi kuhusianan na kifo chake zikidai kuwa mijitu yenye roho mbaya kama ya shetani ilimkomba marehemu kila kitu alichokuwa nacho na kuuacha mwili wake ukiwa na pensi ya ndani tu maarufu kama 'boxer'.

Mbunge Mtangi aliyekuwa mmoja wa watu walioguswa sana na taarifa hizo, aliibukia kwenye viunga vya Hospitali ya Muheza na kuungana na wananchi kibao ambao nao walifika hapo kuthibitisha kama kweli msanii huyo kipenzi cha wengi ameaga dunia kwa kujeruhiwa kichwani kufuatia ajali mbaya ya kupinduka zaidi ya mara tatu kwa gari alilokuwa akiendesha na kuharibika vibaya aina ya Toyota Harrier.

Baadaye, umati wa watu ulipozidi, mhudumu wa chumba cha maiti hospitalini hapo aliyetambulika kwa jina la Mhusa na pia daktari mmoja aitwaye Kibaja walilazimika kuomba msaada wa walinzi hospitalini hapo ii kuzuia umati huo usiingie kwa wakati mmoja na kuathiri shughuli za utoaji huduma na masomo kwa wanafunzi wanaosomea udaktari.

Sharomilionea alipata ajali hiyo wakati akiwa katika Kijiji cha Mguzoni wilayani Muheza, mkoani Tanga kuelekea kwao katika Kijiji cha Lusanga, wilayani humo humo (Muheza) kwa nia ya kuwajulia hali wazazi wake.

Baada ya kupata ajali mbaya na kufariki, mijitu yenye roho ya shetani haikujishughulisha na hatua yoyote ya kuukimbizia mwili wake hospitali bali walianza kumkomba kila kitu na mwishowe kumsaula viwalo vyake na kutokomea navyo, wakimuacha na nguo ya ndani tu.

KAMPUNI YA AIRTEL
Kampuni ya huduma za simu ya Airtel ambayo hivi karibuni imkuwa ikipata mafanikio makubwa katika kutoa matangazo yake kupitia Sharomilionea, imeguswa na kifo cha msanii huyo na kutoa ujumbe maalum wa kumkumbuka.

Katika kuelezea hisia zao, Airtel wameandaa bango maalum la kumkumbuka, likiwa na picha yake yenye pozi 'tamu' na kuandika juu yake ujumbe wenye maandishi makubwa yasemayo: "Daima utakumbukwa kjwa ucheshi na upendo wako, hakuna atakayeziba pengo lako."

Katika tangazo mojawapo lililokimbiza sana la Airtel, Sharomilionea anaonekana akimtamkia kwa mbwembwe msanii mwingine, King Majuto kwa kumwambia 'Umebuugi meeen...!" , ambapo sasa msemo huo ni miongoni mwa matamshi yasiyokauka midomoni mwa vijana wengi wa mjini.

No comments:

Post a Comment