Sunday, May 19, 2013

SH. MILIONI 500 ZAPATIKANA MECHI YA SIMBA, YANGA

Nahodha Nadir Haroub 'Cannavaro' akibeba taji la ubingwa wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya mechi yao waliyoshinda 2-0 dhidi ya Simba kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

MECHI ya watani wa jadi Simba na Yanga ya Ligi Kuu ya Vodacom iliyochezwa jana (Mei 18 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na kumalizika kwa mabingwa wapya Yanga kushinda mabao 2-0 yaliyofungwa na wachezaji wa kigeni Didier Kavumbagu na Hamisi Kiiza, imeingiza sh. 500,390,000.

Mechi hiyo namba 180 ambayo ilikuwa kati ya saba la kuhitimisha ligi hiyo msimu wa 2012/2013 ilishuhudiwa na watazamaji 57,406 waliokata tiketi kwa viingilio vya sh. 5,000, sh. 7,000, sh. 10,000, sh. 15,000, sh. 20,000 na sh. 30,000.

Kila klabu imepata mgawo wa sh. 123,970,927.45 wakati Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh. 76,330,677.97.

Kiingilio cha sh. 5,000 ndicho kilichovutia watazamaji wengi ambapo waliokata tiketi hizo walikuwa 19,039 na kuingiza sh. 95,195,000 wakati kile cha sh. 7,000 kiliingiza watazamaji 17,647 na kupatikana sh. 123,515,000.

Mgawo mwingine wa mapato hayo ni asilimia 15 ya uwanja sh. 63,036,064.81, tiketi sh. 3,818,890, gharama za mechi sh. 37,821,638.88, Kamati ya Ligi sh. 37,821,638.88, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 18,910,819.44 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 14,708,415.12.

Saturday, May 18, 2013

RATIBA LIGI KUU ZA ULAYA


LIGI KUU YA ENGLAND

JUMAPILI, Mei 19
Chelsea              v Everton             saa (12:00) jioni  
Liverpool            v Queens Park Rangers saa (12:00) jioni  
Manchester City      v Norwich City        saa (12:00) jioni  
Newcastle United     v Arsenal             saa (12:00) jioni  
Southampton          v Stoke City          saa (12:00) jioni  
Swansea City         v Fulham              saa (12:00) jioni  
Tottenham Hotspur    v Sunderland          saa (12:00) jioni  
West Bromwich Albion v Manchester United   saa (12:00) jioni  
West Ham United      v Reading             saa (12:00) jioni  
Wigan Athletic       v Aston Villa         saa (12:00) jioni


LIGI KUU YA HISPANIA (La Liga)

JUMAMOSI, Mei 18
Getafe           v Valencia        saa (1:00) usiku  
Granada CF       v Osasuna         saa (3:00) usiku  
Sevilla          v Real Sociedad   saa (5:00) usiku  
 
JUMAPILI, Mei 19
Levante          v Rayo Vallecano  saa (7:00) mchana  
Deportivo Coruna v Espanyol        saa (12:00) jioni  
Real Zaragoza    v Athletic Bilbao saa (2:00) usiku  
Barcelona        v Real Valladolid saa (4:00) usiku 
 
JUMATATU, Mei 20
Real Mallorca    v Real Betis      saa (5:00) usiku


LIGI KUU YA UJERUMANI (Bundesliga)

JUMAMOSI, Mei 18
Nuremberg                 v Werder Bremen       saa (10:30) alasiri  
Borussia Dortmund         v Hoffenheim          saa (10:30) alasiri  
Borussia Moenchengladbach v Bayern Munich       saa (10:30) alasiri  
Eintracht Frankfurt       v VfL Wolfsburg       saa (10:30) alasiri  
FC Augsburg               v Greuther Fuerth     saa (10:30) alasiri  
Hamburg SV                v Bayer Leverkusen    saa (10:30) alasiri  
Hanover 96                v Fortuna Duesseldorf saa (10:30) alasiri  
Freiburg                  v Schalke 04          saa (10:30) alasiri  
VfB Stuttgart             v Mainz               saa (10:30) alasiri


LIGI KUU YA ITALIA (Serie A)

JUMAMOSI, Mei 18Sampdoria        v Juventus                        saa (3:45) usiku 

JUMAPILI, Mei 19
Atalanta Bergamo v Chievo Verona         saa (10:00) usiku 
Bologna          v Genoa                           saa (10:00) usiku
Torino           v Catania                           saa (10:00) usiku
AS Roma          v Napoli                        saa (3:45) usiku 
Cagliari         v Lazio                               saa (3:45) usiku  
Inter Milan      v Udinese                         saa (3:45) usiku 
Palermo          v Parma                           saa (3:45) usiku 
Pescara          v Fiorentina                       saa (3:45) usiku
Siena                          v AC Milan         


LIGI KUU YA UFARANSA (Ligue 1)
    
JUMAMOSI, Mei 18
AS Nancy                 v Bastia              saa (4:00) usiku  
ES Troyes AC             v Girondins Bordeaux  saa (4:00) usiku  
Evian Thonon Gaillard FC v Valenciennes        saa (4:00) usiku  
Sochaux                  v Toulouse            saa (4:00) usiku  
Montpellier HSC          v Lille               saa (4:00) usiku  
Nice                     v Olympique Lyon      saa (4:00) usiku  
Paris St Germain         v Stade Brest         saa (4:00) usiku  
Stade Rennes             v Ajaccio             saa (4:00) usiku  
St Etienne               v Olympique Marseille saa (4:00) usiku  
Stade de Reims           v FC Lorient          saa (4:00) usiku

Friday, May 17, 2013

BIG BROTHER YAREJEA, KUZINDULIWA JUMAPILI MEI 26

Logo mpya ya Big Brother The Chase 2013
Mtangazaji wa Big Brother, IK.


SHOO kubwa zaidi Afrika ya Big Brother imerejea katika msimu wake 8 mara hii ikienda kwa jina la The Chase.

Washiriki 28 kutoka nchi 14 za Afrika watakuwa wakifukuzia sit u zawadi ya kwanza ya dola 300 000 za Marekani lakini pia kupata umaarufu na hata kutafuta wenza. 

Msimu mpya wa Big Brother The Chase utazinduliwa Jumapili Mei 26 na itajumuisha mabadiliko mengo na ‘surprise’ kubwa ambazo zitahitaji washiriki kutumia werevu wao ili kusonga mbele.

Habari nzuri za ziada ni kwamba mburudishaji IK Osakioduwa kwa mara nyingine atarejea kuwa muongozaji wa shindano hilo la mwaka 2013 la The Chase. Amekuwa kipenzi cha mashabiki wengi kote Afrika kutokana na uwezo wake kuzungumza kwa uwazi na washiriki na kuwasaidia kuchukulia poa vipindi vyao vigumu.

Kwa siku 91, shoo hiyo kubwa Afrika itaonyeshwa ‘live’ kwa saa 24 za siku zote 7 za wiki katika channel 197 na 198 za DStv.

JIJI LA DAR ES SALAAM LINAVYOONGOZA KWA USAFI...

Maji taka yakitiririka na kutapakaa katika mitaa ya India na Indiraghandi Jijini Dar es Salaam huku Mchoma viazi vitamu na watembea kwa miguu wakipita katika maji hayo kitu ambacho ni hatari kwa afya ya wakazi wa maeneo hayo (Picha na Eleuteri Mangi – MAELEZO).

SIMBA, YANGA KUFUNGA PAZIA LIGI KUU J'MOSI

Wachezaji wa Simba (juu) na wa Yanga (chini) wakishangilia katika mechi zao tofauti za Ligi Kuu ya Tanzania Bara msimu huu. Nani atacheka Jumamos hiii?


Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kuwania ubingwa wa Tanzania Bara msimu huu (2012/2013) inafikia tamati kesho (Mei 18 mwaka huu) kwa timu zote 14 kupambana katika viwanja saba tofauti.

Mechi zote zitachezwa kuanzia saa 10 kamili jioni. Ni jukumu la kamishna wa mechi husika kuhakikisha mchezo unaanza katika muda uliopangwa, vinginevyo hatua za kinidhamu zitachukuliwa kwa mujibu wa Kanuni za Ligi Kuu ya Vodacom toleo la 2012.

Yanga ambayo tayari imeshatwaa ubingwa itakuwa mgeni wa Simba katika mechi namba 180 itakayochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ambapo mwamuzi atakuwa Martin Saanya kutoka Morogoro na Kamishna ni Emmanuel Kavenga wa Mbeya.

Mgambo Shooting vs African Lyon (Uwanja wa Mkwakwani, Tanga. Mwamuzi ni Amon Paul wa Mara wakati Kamishna ni Ally Mkomwa kutoka Pwani), JKT Ruvu vs Mtibwa Sugar (Uwanja wa Azam Chamazi, Dar es Salaam. Mwamuzi ni Israel Mujuni wa Dar es Salaam wakati Kamishna ni Salum Kikwamba kutoka Kilimanjaro).

Tanzania Prisons vs Kagera Sugar (Uwanja wa Sokoine, Mbeya. Mwamuzi ni Ibrahim Kidiwa wa Tanga wakati Kamishna ni John Kiteve kutoka Iringa), Oljoro JKT vs Azam (Uwanja wa Sheikh Kaluta Amri Abeid, Arusha. Mwamuzi ni Athuman Lazi wa Morogoro wakati Kamishna ni Juma Mgunda kutoka Tanga).

Uwanja wa Jamhuri, mjini Morogoro utatumika kwa mechi kati ya Polisi Morogoro na Coastal Union ya Tanga ambapo Mwamuzi atakuwa Said Ndege wa Dar es Salaam wakati Kamishna ni Hakim Byemba kutoka Dodoma. Toto Africans itacheza na Ruvu Shooting katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza ambapo mwamuzi ni Geoffrey Tumaini kutoka Dar es Salaam na Kamishna ni Josephat Magazi wa Singida.

MECHI ZA MARUDIANO RCL KUPIGWA WIKIENDI HII


Mechi za marudiano za raundi ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa wa Mikoa (RCL) zinachezwa wikiendi hii katika viwanja kumi tofauti wakati mechi ya Flamingo ya Arusha na Machava FC ya Kilimanjaro yenyewe itachezwa Jumatatu (Mei 20 mwaka huu).

Uamuzi wa mechi hiyo kuchezwa Jumatatu ni kutokana na Uwanja wa Sheikh Kaluta Amri Abeid kutumika kwa mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kesho wakati Jumapili utatumika kwa shughuli nyingine za kijamii kwa mujibu wa wamiliki wa uwanja huo (CCM Mkoa wa Arusha).

Mechi nyingine zitachezwa keshokutwa (Jumapili) ambapo Abajalo watakuwa wenyeji wa Red Coast kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Dar es Salaam. Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara utatumika kwa mechi kati ya wenyeji Coast United na Kariakoo ya Lindi.

African Sports ya Tanga itaoneshana kazi na Techfort ya Ifakara mkoani Morogoro katika mchezo utakaochezwa Uwanja wa Mkwakwani. Nayo Simiyu United ya Simiyu itakuwa mgeni wa Magic Pressure ya Singida kwenye Uwanja wa Namfua, mjini Singida.

Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza ndiyo utakaotumika kuzikutanisha timu za Polisi Jamii Bunda kutoka Mara na wenyeji UDC wakati Biharamulo FC ya Kagera na Polisi SC ya Geita zitaumana kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.

Milambo FC ya Tabora itakuwa mwenyeji wa Saigon FC ya Kigoma kwenye Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora huku Mbinga United ya Ruvuma ikiikaribisha Njombe Mji ya Njombe kwenye Uwanja wa Majimaji mjini Songea.

Uwanja wa Kumbukumbu ya Samora mjini Iringa utatumika kwa mechi kati ya wenyeji 841 KJ dhidi ya Kimondo SC kutoka Mbeya. Nazo Rukwa United na Katavi Warriors zitapimana ubavu kwenye Uwanja wa Nelson Mandela mjini Sumbawanga.

Timu zitakazofuzu kucheza raundi ya pili zitacheza mechi zao za kwanza kati ya Mei 25 na 26 mwaka huu wakati mechi za marudiano ni kati ya Juni 1 na 2 mwaka huu.

MSHINDI WA SH. MILIONI 100 ATUA DAR KUPOKEA MAHELA YA VODACOM

Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania, Matina Nkurlu (katikati) akiongea na mshindi wa droo kubwa ya "MAHELA" Valerian Nickodemus (22) (kulia) baada ya kuwasili katika kituo cha mabasi cha Ubungo jijini Dar es Salaam akitokea Mkoa wa Kigoma kuja kukabidhiwa fedha zake taslimu hivi karibuni Sh. milioni 100. Anayeshuhudia kushoto ni mmoja wa wafanyakazi wa kituo cha mabasi Ubungo.

Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania, Matina Nkurlu (katikati) akiongea na mshindi wa droo kubwa ya "MAHELA" Valerian Nickodemus (22) (kulia) baada ya kuwasili katika kituo cha mabasi cha Ubungo jijini Dar es Salaam akitokea Mkoa wa Kigoma kuja kukabidhiwa fedha zake taslimu hivi karibuni Sh. milioni 100. Anayeshuhudia kushoto ni mmoja wa wafanyakazi wa kituo cha mabasi Ubungo.
Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania, Matina Nkurlu (kushoto) akiongozana na mshindi wa droo kubwa ya "MAHELA" Valerian Nickodemus (22) (kulia) baada ya kuwasili katika kituo cha mabasi cha Ubungo jijini Dar es Salaam akitokea Mkoa wa Kigoma kuja kukabidhiwa fedha zake taslimu hivi karibuni Sh. milioni 100.

Mshindi wa droo kubwa ya "MAHELA", Valerian Nickodemus (kushoto) akimsikiliza kwa umakini mwandishi wa habari wa ITV Emanuel Buhohela mara baada ya kuwasili katika kituo cha mabasi cha Ubungo jijini Dar es Salaam akitokea Mkoa wa Kigoma mahususi kwa ajili ya makabidhiano rasmi ya fedha zake Sh. Milioni 100 hivi karibuni. Kulia ni Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania, Matina Nkurlu.

Mshindi wa droo kubwa ya "MAHELA", Valerian Nickodemus (katikati) akikaribishwa na Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania, Matina Nkurlu (kulia) mara baada ya kuwasili katika kituo cha mabasi cha Ubungo jijini Dar es Salaam akitokea Mkoa wa Kigoma mahususi kwa ajili ya makabidhiano rasmi ya fedha zake Sh. Milioni 100 hivi karibuni.