Msanii nyota wa
Marekani, Rihanna ameendelea kuwa ‘bize’ katika ziara zake za kula bata katika
maeneo mbalimbali yanayosifika kwa kuponda maraha duniani.
Akiwa na rundo la
wapambe wake, Rihanna ameshajirusha sana katika maeneo ya kujidai ya jiji la
New York, akaenda zake Barbados, akatua nchini Italia na sasa yuko katika fukwe
za kusini mwa Ufaransa, akiendelea kujiachia kupita kiasi na wapambe wake ndani
ya boti ya kifahari.
Tazama baadhi ya mapicha
yake aliyopigwa jana wakati yeye na wenzake wakila, kukata kilaji, kuvuta
sigara, kuimba, kukata mauno sanaaaa na kasha kujimwaga baharini na vijaketi
maalum vya kuogelea na pia kuendesha ‘pikipiki’ za baharini.
 |
Yanawahu? Fuata nyuki upate manundu |
 |
Mchumu mchumu, mchumu tena....mmwaaa! |
 |
Chezea Rihanna weye... nani anamuweza kwa mauno? |
 |
We unageuka kwangu kuna nini? Si uendelee na mambo yako! |
 |
Hapa Rihanna keshaanza kuwa bwaksi....bila shaka anaimba: "... nataka paja miee.. hakinitoshi kipapatio! |
 |
Hapa mrembo kakalia nini? Kigoda cha Rihanna! |
 |
Usiangalie utapofuka! |
 |
Mitungiii, blantiii, mikasii...ooh yeah! |
 |
Wewweeeeeehhh....! |
 |
Twende nikupe lifti |
No comments:
Post a Comment