Friday, July 6, 2012

UNAJUA TEKNOLOJIA YA GOLI INAVYOFANYA KAZI? SOMA HAPA

*Ligi Kuu ya England kuanza kuitumia msimu huu 2012-13

John Terry wa England akiosha wavuni goli la Ukraine ambalo halikuhesabiwa wakati wa mechi yao ya hatua ya makundi ya Euro 2012. Ukraine walilala 1-0.

 

ZURICH, Uswisi
TEKNOLOJIA ya mstari wa goli huenda ikaanza kutumika kwenye Ligi Kuu ya England katikati ya msimu huu wa 2012-13 baada ya Bodi ya Kimataifa ya Kusimamia Mchezo wa Soka (IFAB) kuidhinisha matumizi ya teknolojia viwanjani mjini Zurich.

Aina mbili za teknolojia - Jicho la Mwewe (Hawk-Eye) na Refa wa Lango (GoalRef) - zimepitishwa na FIFA kutumika.

Teknolojia inatumika kwa mara ya kwanza kwenye fainali za Kombe la Dunia la Klabu la FIFA Desemba na, kama itaonyesha mafanikio, itatumika katika Kombe la Shirikisho 2013 na Kombe la Dunia 2014. 

Ligi Kuu ya England imesema inataka kuanza kutumia teknlojia "haraka iwezekanavyo."

Taarifa ya Ligi Kuu ya England kufuatia ruhusa hiyo ya IFAB imesema: "Ligi Kuu ya England imekuwa ikiitaka teknolojia ya goli la mstari kwa muda mrefu.

Katibu Mkuu wa chama cha soka cha England (FA), Alex Horne amesema: "Tunayakaribisha maamuzi haya yaliyotolewa leo na IFAB na tunaingia katika mijadala ya kuamua kutumia teknolojia zote Jicho la Mwewe (Hawk-Eye) na Refa wa Goli (GoalRef) hivi karibuni ili tuanze kuitumia haraka iwezekanavyo."

Horne alisema FA itaamua muda wa kuanza kutumia teknolojia.
"Inaweza kuwa ni Desemba wakati teknolojia itakapokuwa imeshathibitishwa rasmi na kusimikwa," alisema katika mkutano na waandishi wa habari mjini Zurich. "Kipaumbele ni kuanza kutimika katika Kombe la Dunia la FIFA nchini Japan.

"Ligi Kuu ya England inahitaji kuzungumza na kampuni mbili zilizopewa haki za kusambaza teknlojia hiyo na klabu za ligi. Kwa ninachofahamu ni kwamba klabu zinasapoti, na kwa maana hiyo, kama klabu zote zitakubali itaanza kutumika katikati ya msimu, au kabla ya kuanza kwa msimu wa 2013-14."

Dhamira ya kutaka kuleta teknolojia ya goli iliongezeka baada ya Ukraine kunyuimwa goli lao halali la kusawazisha baada ya mpira kuvuka mstari wa lango katika mechi waliyolala 1-0 dhidi ya England katika fainali za Euro 2012.

Kocha wa Chelsea, Roberto Di Matteo amesema: "Tunashuhudia kila msimu, kila kwenye michuano mikubwa, tunahitaji teknlojia hii kwa sababu kuna matukio muhimu mno wakati wa mechi hizo ambapo unaweza kupata suluhisho sahihi kwa kutumia teknolojia."

Rais wa UEFA, Michel Platini anaaminika kwamba anapenda zaidi kutumia waamuzi watano, jambo ambalo limeidhinishwa na FIFA jana.

Mfumo huo, ambao unawashuhudia mwamuzi wa ziada akisimama kwenye kila mstari wa goli na kuzunguka eneo la penalti, umekuwa katika majaribio tangu mwaka 2008 na ulitumika pia wakati wa Euro 2012 pamoja na Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya.

FIFA pia imeondoa katazo wanawake kucheza soka wakiwa wamevaa hijab, jambo linaloruhusu mataifa yenye imani ya dini ya Kiislamu kushiriki michuano mikubwa.




JICHO LA MWEWE LINAFANYAJE KAZI?

Teknolojia ya Jicho la Ndege Tai (Hawk-Eye) inatumia kamera sita, zinazoelekea kwenye kila lango, kuufuatilia mpira uwanjani.

Mfumo huo unatumia kitu kinaitwa "pembetatu" kubaini mpira uko mahala gani hasa.

Kama mpira utavuka mstari wa lango, "ishara" itatumwa kwenye saa ya mkononi ya refa kuashiria kuwa goli limetinga.

Kwa matakwa ya FIFA, tukio hilo zima litatumia chini ya sekunde kukamilika.
 
TEKNOLOJIA YA "GOAL REF" INAFANYAJE KAZI? 


Teknolojia ya "GoalRef" inatumia ki-chip kidogo kinachopandikizwa kwenye mpira na inatumia miale ya sumaku langoni.

Mfumu huo utabaini mabadiliko katika miale ya sumaku ndani ama nje ya lango kutambua kama goli limefungwa.

Tukio hilo zima linatumia muda wa chini ya sekunde moja, na majibu yanamwendea refa kwa umeme refa.
 

No comments:

Post a Comment