Basi la Yanga |
Tukio hilo limetokea kwenye jukwaa la kusini mwa Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga wakati wa mechi ya Ligi Kuu ya Bara kati ya wenyeji JKT Mgambo na Azam ambapo shabiki mmoja aliyevalia jezi ya Yanga, alivuliwa wakati wa mapumziko na kisha jezi hiyo ikachomwa moto huku wengine wakishangilia na kupiga makofi.
Mbaya zaidi, mashabiki hao waliokuwa akifurahia kitendo hicho hawakuonekana kufanya jiotihada zozote za kumvisha mtu waliyemvbua jezi hiyo ambaye kwa dakika kadhaa alionekana akiwa tumbo wazi na kujawa na fadhaa kubwa huku wapinzani wake wakimcheka na kuapiza kuwa piga ua, lazima 'Wanajangwani' watachezea kichapo kesho katika mechi yao ya mwisho ya mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu ya Bara dhidi ya wenyeji Coastal Union.
Juzi, basi la Yanga lilipigwa mawe na watu wanaodhaniwa kuwa ni mashabiki wa Simba na kioo kimojawapo kikapasuka na inasemekena kuwa straika Simkon Msuva wa vinara hao wa ligi kuu ya Bara alipata jeraha.
Yanga watashuka dimbani kwenye Uwanja wa Mkwakwani kesho huku wakijua kwamba matokeo yoyote watakayopata hayatawaathiri kwenye msimamo wa ligi kwani hadi sasa wanaongoza kwa kuwa na pointi 26 baada ya kucheza mechi 12, pointi mbili zaidi ya Azam waliopokea kipigo kisichotarajiwa cha mabao 2-1 kutoka kwa Azam na pointi tatu zaidi ya mahasimu wao wa jadi, Simba waliochezea kichapo cha bao 1-0 kutoka kwa Toto African ya Mwanza.
Roho zao mbaya Saana Hawa
ReplyDelete