Saturday, November 10, 2012

CHICHARITO APIGA 'HAT-TRICK' MAN U IKIPAA KILELENI NA KUZIACHA KWA TOFAUTI YA POINTI 4 ... ARSENAL YAKOSA PENATI DAKIKA YA 90 NA KUSHIKILIWA KWA SARE YA 3-3...!

Goooooohhh....! Chicharito akishangilia moja kati ya mabao yake matatu aliyofunga dhidi ya Aston Villa na kuipa Man U ushindi wa 3-2 katika mechi yuao ya Ligi Kuu ya England leo Nov. 10, 2012.

Chukua mpira wako mwana... unatisha! Chicharito akipongezwa na mchezaji mwenzake wa Man U, Antonio Valencia baada ya kuopiga 'hat-trick' na kuipa timu yake ushindi wa 3-2 dhidi ya Aston Villa leo Nov. 10, 2012

Chicharito wa Man U akifunga goli lake la pili dhidi ya Aston Villa leo Novemba 10, 2012.Mtokea benchi Javier Hernandez 'Chicharito' amekuwa shujaa wa Man U usiku huu baada ya kupiga 'hat-trick' na kuisaidia klabu yake kuibuka na ushindi wa 3-2 dhidi ya Aston Villa na kujichimbia kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu ya England kwa tofauti ya pointi 4 dhidi ya wapinzani wao Chelsea wanaocheza kesho dhidi ya Liverpool na pia mahasimu wao wa jadi, Man City watakaowavaa Tottenham kesho.

Villa walitangulia kuongoza kwa mabao 2-0 kabla kocha wao Alex Ferguson hajaonyesha 'maujuzi' yake kwa kumuingiza Chicharito badala ya Ashley Young.

Mara tu alipoingia, Chicharito ambaye alionyesha kiwango chake cha juu cha kujiweka katika nafasi nzuri za kufunga na kuisawazishia Man U magoli yote kabla hajatumia vyema krosi safi ya Robin Van Persie kwa kufunga kwa kichwa goli la ushindi wakati zikiwa zimesalia dakika tatu kabla muda wa kawaida wa mechi kumalizika.


Ushindi wa usiku huu ni wa tano kwa Man U kuupata msimu huu baada ya kutanguliwa na wapinzani wao msimu huu na Chicharito amefikisha magoli saba katika mechi tano zilizopita.


Katika mechi nyingine leo, Mikel Arteta alikosa penati katika shuti la mwisho la mechi na kuikosesha Arsenal ushindi baada ya kushikiliwa nyumbani kwa sare ya 3-3 dhidi ya Fulham ya kina Dimitar Berbatov aliyetuopia mgoli mawili ya timu yake na kutoa pasi moja ya goli la Fulham.
 

MATOKEO MECHI LIGI KUU ENGLAND LEO J'MOSI NOV 10:
    Arsenal 3 - 3 Fulham
    Everton 2 - 1 Sunderland
    Reading 0 - 0 Norwich
    Southampton 1 - 1 Swansea
    Stoke 1 - 0 QPR
    Wigan 1 - 2 West Brom
    Aston Villa 2 - 3 Man U 


MDIMAMO LIGI KUU ENGLAND BAADA YA MECHI ZA LEO JUMAMOSI NOV. 10, 2012


Played GD Points
1 Man Utd 11 13 27
2 Chelsea 10 12 23
3 Man City 10 9 22
4 Everton 11 7 20
5 West Brom 11 5 20
6 Tottenham 10 3 17
7 Arsenal 11 7 16
8 Fulham 11 5 16
9 West Ham 10 2 15
10 Newcastle 10 -2 14
11 Swansea 11 1 13
12 Stoke 11 -1 12
13 Liverpool 10 -2 11
14 Wigan 11 -6 11
15 Norwich 11 -10 11
16 Sunderland 10 -4 9
17 Aston Villa 11 -7 9
18 Reading 10 -6 6
19 Southampton 11 -14 5
20 QPR 11 -12 4

No comments:

Post a Comment