Monday, July 15, 2013

XAVI APATA JIKO... AMUOA DEMU WAKE WA LONGTAIM KITAMBO NURIA CUNILLERA... MASTAA KIBAO WAHUDHURIA WAKIONGOZWA NA LIONEL MESSI, INIESTA, CESC... FUNGATE LAO BAB'KUBWA KUHITIMISHWA VISIWA VYA SHELISHELI VYA BAHARI YA HINDI BARANI AFRIKA

Xavi na mkewe Nuria wakiwa na furaha baada ya kufungishwa ndoa
Hapo chacha... Xavi na mkewe Nuria baada ya kugongesha glasi
Cheeers...!
Biharusi Nuria Cunillera akipungia mkono watu waliokuwa wakimshangilia wakati akiwasili katika eneo la tukio la harusi yake na Xavi kwenye viunga vya bustani ya Marimurtra botanical, Catalonia nchini Hispania usiku wa kuamkia leo.
Tisha mbaya....! Bwanaharusi Xavi akitinga eneo la tukio kabla ya kufungwa kwa ndoa yake na Nuria.
Picha za maharusi Xavi na Nuria zikichanganywa na za mandhari ya eneo walilofunga ndoa yao usiku wa kuamkia leo
Iniesta na mkewe pia walichangamkia mnuso.
Kipa Victor Valdes na mkewe pia walihudhuria mnuso wa harusi ya Xavi.
Mascherano na mkewe pia hawakutaka kukosa.

Cesc Fabregas na mpenziwe wakiwasili katika eneo la sherehe ya harusi ya Xavi
Singleboy? Beki Jordi Alba alitinga katika eneo la tukio la mnuso wa Xavi akiwa kivyakevyake.
Sergio Busquets pia aliwasili kiugumugumu... bila demu wake wala nini!
Pedro na mpenziwe... wanapendedha eeenh!





Twenzetu...! Iniesta na mkewe
Mshambuliaji David Villa wa Atletico Madrid naye alikuwapo



Xavi na Nuria wakiwa kwenye mtoko enzi zao kabla ya kuoana.

Mtoko mwingine wa Xavi na mkewe Nuria enzi za kuwa wachumba
BARCELONA, Hispania
Kiungo nyota wa Barcelona na timu ya taifa ya Hispania, Xavi Hernández na mchumba wake wa 'longtaim' kitambo, Nuria Cunillera wameoana usiku wa kuamkia leo (Jumapili - Jumatatu) katika sherehe bab'kubwa iliyofanyika kwenye viunga vya bustani ya Marimurtra Botanical, ndani ya kitongoji cha Girona mjini Blanes na kuhudhuriwa na wageni maalum zaidi ya 180, wakiwamo mastaa kibao wa Barca na timu ya taifa ya Hispania.

Shughuli za ufungishaji ndoa zilianza saa 1:30 usiku, na baada ya hapo, maharusi na msafara wao uliosindikizwa na msururu wa wapambe waliokuwa ndani ya mikoko ya bei mbaya ulielekea katika eneo jirani la "El Convent", ndani ya ukumbi mkali wa kisasa wa XVI Century, ambako sherehe ziliendelea kwa saa kadhaa.

Lionel Messi, Iniesta, Victor Valdes, Mascherano na Cesc Fabregas ni miongoni mwa nyota waliohudhuria huku waliokosekana kutokana na sababu mbalimbali zikiwamo za kuwa nje ya nchi wakila bata katika kipindi hiki cha mapumziko ni beki Gerard Piqué na mpenziwe Shakira, Carles Puyol na mpenziwe Vanessa Lorenzo pamoja na rafiki mkubwa wa Xavi, kipa Iker Casillas wa Real Madrid na mpenziwe Sara Carbonero. Hawakuwapo pia makocha na marais wa Barca.

Hata hivyo, ilibainika baadaye kwamba maandalizi ya harusi hiyo yalikuwa ya siri. Baada ya ndoa, Xavi na mkewe walianza safari ya kwenda katika visiwa vya Shelisheli vilivyopo kwenye Bahari ya Hindi barani Afrika ili kufaidi maraha ya fungate.

Xavi anatakiwa kuripoti klabuni Barcelona Julai 29 ambapo ataungana na wenzake katika maandalizi ya msimu mpya wa La Liga, Ligi Kuu ya Hispania.

No comments:

Post a Comment