Wednesday, July 24, 2013

'NEYMAR ATAFULIA BARCA KAMA IBRA'

Neymar

BARCELONA, Hispania
KOCHA wa zamani wa AC Milan, Arrigo Sacchi (67) anaona kwamba mchezaji mpya wa Barcelona, Neymar anaweza kushindwa kung'aa klabuni hapo kama ilivyomtokea Zlatan Ibrahimovic, ambaye aliishia kuhama baada ya kuichezea klabu hiyo ya Hispania kwamsimu mmoja tu 2009 .

"Sijui ni kivipi Neymar atafanikiwa Barcelona. Pale Barca, staili ya kucheza ni muhimu kuliko chochote. Tusubiri tuone kama Neymar atafiti pale," Sacchi alisema.

"Ninachosema ni kwamba huwezi kujua ni vipi mambo yatamwendea. Hebu angalia kilichomtokea Ibrahimovic. Alikuwa na kipaji chote cha kuchezea Barca, lakini mwishowe alishindwa kufiti kikosini na wachezaji wenzake."

No comments:

Post a Comment