Wednesday, July 24, 2013

DE BRYUNE WA CHELSEA KUFANYIWA 'SCAN'

De Bruyne

KUALA LUMPUR, Malaysia
MSHAMBULIAJI mpya wa Chelsea, Kevin de Bruyne anarejea London kwa ajili ya kufanyiwa 'scan' baada ya kuumia goti katika mechi ya kirafiki Jumapili waliyoshinda 4-1 dhidi ya Malaysia XI mjini Kuala Lumpur.

Baada ya kupika goli la kwanza, Mbelgiji huyo aliumia wakati akifunga goli la pili la timu yake kwenye Uwanja wa Shah Alam.

De Bruyne (22), alifunga vyema kwa mpira wa kuunganisha moja kwa moja lakini alianguka vibaya na haraka akaita kuomba msaada.

No comments:

Post a Comment