Friday, July 19, 2013

NEYMAR APEWA JEZI YA THIAGO ALCANTARA

Neymar siku ya utambulisho Barcelona
Jezi yake mgongoni haikuwa na namba.

BARCELONA imetangaza kwamba Neymar atavaa jezi Na. 11 msimu ujao. Na tayari jezi hizo zinauzwa kama njugu katika duka kuu la Barcelona lililopo Nou Camp.

Jambo hili linamaanisha kwamba Mbrazil huyo atavaa jezi iliyoachwa na mchezaji wa timu ya taifa ya vijana ya U-21 ya Hispania, Thiago Alcantara, ambaye ameondoka na kwenda kujiunga na Pep Guardiola klabuni Bayern Munich.

Licha ya kutambulishwa klabuni hapo zaidi ya mwezi uliopita, ilikuwa haijafahamika Neymar atavaa jezi namba ngapi.

Kuondoka kwa Thiago na David Villa kumeacha wazi jezi Na. 11 na 7, ambazo zote Neymar alikuwa akizivaa katika timu yake ya taifa ya Brazil, lakini sasa amechagua Na.11.

No comments:

Post a Comment