Friday, July 19, 2013

HATUMUHITAJI TENA ROONEY, YASEMA PSG

Rooney

KOCHA wa PSG, Laurent Blanc amemwagia maji baridi uvumi unaoihusisha klabu hiyo na mipango ya kutaka kumsajili mshambuliaji wa Manchester United, Wayne Rooney.

Kufuatia usajili waliofanya wa Edinson Cavani kwa euro milioni 63 [paundi milioni 54.4], Blanc amesema kuwa anaona kwamba ameenea vyema mbele na ataongeza kiungo tu kama PSG itarejea sokoni.

Akizungumza na waandishi wa habari, Blanc alisema: "Wayne Rooney ni mchezaji mzuri sana lakini tumekamilika sana katika mashambulizi.

"Tunahitaji kuona tutafanya nini katika kiungo. Kama kuna mchezaji mwingine atakuja, atakuwa ni wa sekta hiyo."

Rooney amekuwa akihusishwa vikali na mipango ya kuondoka Old Trafford, huku PSG, Arsenal na Chelsea zote zikipewa nafasi ya kumnasa nyota huyo mwenye umri wa miaka 27.

Lakini rais wa PSG, Nasser Al-Khelaifi alibainisha Jumatano kwamba Rooney alikuwa akiangaliwa kama mbadala wa Cavani endapo wangemkosa nyoya huyo wa Uruguay, huku pia Man United imeshakataa ofa ya kutoka Chelsea wanaomtaka Rooney.

Aidha, PSG wanatarajiwa kukamilisha usajili wa beki Marquinhos mwenye umri wa miaka 19 kutoka Roma kwa ada ya uhamisho inayokadiriwa kuwa paundi milioni 26 baada ya Mbrazil huyo kupanda ndege kwenda kupima afya mjini Paris.

No comments:

Post a Comment