Friday, July 19, 2013

THAMANI YA SUAREZ NI KAMA YA CAVANI, ASEMA KOCHA LIVERPOOL

Luis Suarez (kulia) akiwa na Edinson Cavani wakati wakiitumikia timu ya taifa ya Uruguay

BRENDAN Rodgers bado anaamini kwamba Liverpool itambakisha Luis Suarez katika kipindi hiki cha usajili, na amesema ofa yoyote kwa ajili ya mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 26 inapaswa kuwa sawa na ile ambayo PSG walilipa kumpata Muuruguay mwenzake Suarez, Edinson Cavani.

Rodgers anaamini kwamba mshambuliaji huyo anayetaka kuondoka ni kati ya wachezaji bora zaidi duniani na amesema ofa yoyote kwa Suarez inapaswa kuakisi kipaji chake, ingawa Rodgers bado anaamini kwamba atambakisha Suarez Anfield.

"Unapozingatia kwamba Cavani ameondoka kwa paundi milioni 55 unajua ... Luis ana kipaji cha matawi hayo hayo," Rodgers aliliambia gazeti la Liverpool Echo. "Kiufupi ofa iliyokuja (kutoka Arsenal) tuliona hailingani na thamani ya kipaji chake, na hata kama wakija tena na kiasi hicho cha pesa, haina garantii kwamba atauzwa kwa sababu tunajaribu kujenga kitu  hapa."

Rodgers anaona kwamba Liverpool iko katika hali ambayo haioni ulazima wa kumuuza mshambuliaji huyo mtata.

"Tunakontroo yote ya suala lake, hatulazimiki kumuuza," Rodgers alisema. "Ana miaka mitatu imebaki katika mkataba wake.

"Tunajiandaa kuleta wachezaji wapya na kutumia pesa bila ya kuhitaji kumuuza Luis Suarez."

No comments:

Post a Comment