Friday, July 19, 2013

LYON YAKANUSHA KUMTAKA GERVINHO

Gervinho

KOCHA wa Lyon, Remi Garde amekanusha uvumi kwamba klabu yake inajiandaa kumsajili Gervinho kutoka Arsenal kwa kubadilishana naye na kiungo Yoann Gourcuff.

Ilibainishwa Jumatano kwamba Roma wametuma ofa ya paundi milioni 6.9 kwa ajili ya kutaka kumsajili mshambuliaji huyo wa Ivory Coast lakini ripoti nchini Ufaransa zilidai kwamba Lyon pia wanamhitaji nyota huyo mwenye umri wa miaka 26.

Hata hivyo, Garde alisisitiza kwamba dili la kubadilishana wachezaji baina ya Gervinho na Gourcuff ambaye analipwa pesa nyingi zaidi klabuni Lyon, ni uvumi tu.

"Taarifa hizo hazitoki kwetu. Nimezisoma magazetini tu," Garde alisema. "Gervinho ni mshambuliaji. Tunao washambuliaji, yosso wa ubora wa juu."

No comments:

Post a Comment