Friday, July 19, 2013

ARSENAL KUTUMA OFA YA PAUNDI MIL.40 KWA SUAREZ

Luis Suarez

ARSENAL watatuma ofa iliyoboreshwa ya paundi milioni 40 kwa ajili ya kutaka kumsajili mshambuliaji wa Liverpool, Luis Suarez ndani ya saa 48.

Kocha Arsene Wenger anajiandaa kutuma ofa hiyo baada ya ofa yao ya awali ya paundi 35 kukataliwa, ambapo sasa wameongeza paundi milioni 5 ambazo zitalipwa kwa vipengele.

Vyanzo vimesema kocha huyo wa Arsenal atafanya kila jitihada kuhakikisha anamsajili nyota huyo wa Liverpool katika kipindi hiki cha usajili.

Ilibainishwa kwamba ofa ya awali ya Arsenal ilikataliwa ambayo ilikuwa ni ya paundi milioni 30 na ziada ya paundi milioni 5 ambazo zingelipwa kwa vipengele.

Arsenal sasa wanajiandaa kuikangia kikamilifu katika mbio za kumsajili Suarez, ambaye amekuwa ndiye dhamira kuu ya Wenger wakati akijaribu kusajili wachezaji wenye majina makubwa.

No comments:

Post a Comment