Friday, July 19, 2013

JOVETIC KUPIMWA AFYA MAN CITY LEO, NEGREDO NAYE ALIFUZU VIPIMO JANA

Jovetic

MANCHESTER City watamfanya mshambuliaji Fiorentina, Stevan Jovetic kuwa mchezaji wao wa nne kumsajili katika kipindi hiki cha uhamisho, kama atafuzu vipimo vya afya leo.

Man City haraka wanakamilisha uhamisho unaogharimu paundi milioni 22 wa mchezaji huyo wa kimataifa wa Montenegro wakati kocha mpya Manuel Pellegrini akiendelea kuijenga tuimu yake.

Jovetic (23), alizivutia pia Arsenal na Manchester United.

 

Negredo

Man City pia wametangaza kumsajili mshambuliaji wa Sevilla, Alvaro Negredo baada ya kufuzu vipimo vya afya jana.

Kutua kwa Jovetic na Negredo (27), ambaye alifunga magoli 26 katika La Liga msimu uliopita, Man City watafanya jumla ya pesa walizotumia kusajili katika kipindi hiki cha uhamisho chini ya Pellegrini kufikia paundi milioni 90.

Tayari wameshawasajili Jesus Navas kutoka Sevilla kwa paundi milioni 14.9 na Fernandinho kutoka Shakhtar Donetsk kwa paundi milioni 30.

Jovetic alifunga magoli 13 katika mechi 31 za Fiorentina msimu uliopita na watamsaidia Pellegrini kuziba pengo lililoachwa na kuondoka kwa Mario Balotelli na Carlos Tevez.

No comments:

Post a Comment