Friday, June 7, 2013

MIKOA KIBAO KUPATA WAREMBO WAO WIKIENDI HII


KINYANG’ANYIRO cha Redd’s Miss Tanzania kinazidi kushika kasi ambapo leo mikoa kadhaa inatarajiwa kupata wawakilishi wao.

Kazi kubwa itakuwa kumsaka Redd’s Miss Mbeya, Redd’s Miss Arusha, Redd’s Miss Kigoma na Redd’s Miss Shinyanga ikiwa ni safari ya kuelekea Redd’s Miss Tanzania.

Katika shindano la Redd’s Miss Mbeya kunatarajiwa kuwa na upinzani mkubwa kutoka kwa warembo katika kinyang’anyiro hicho kinachotarajiwa kufanyika kwenye Ukumbi wa City Pub, huku burudani ikitolewa na Linux.

Macho na masikio ya wapenzi wengi pia yataelekezwa katika Redd’s Miss Arusha litakalofanyika katika Ukumbi wa Tripple A na burudani ikitolewa na kundi la muziki la taarabu la Jahazi.

Warembo zaidi ya kumi pia wanatarajiwa kupanda jukwaani ndani ya ukumbi wa NSSF, kwa ajili ya kumpata Redd’s Miss Kigoma, shindano ambalo limekuwa gumzo kubwa mkoani humo.

Redd’s Miss Shinyanga na yenyewe inatarajiwa kufanyika katika Ukumbi wa Rocken Hill, huku burudani ikitolewa na Judith Wambura ‘Lady Jaydee’ aliye maarufu pia kwa jina la Komando.

Shindano la Redd’s Miss Tanzania kwa sasa linadhaminiwa na kinywaji cha Redd’s Original kinachozalishwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL).

Warembo 11 kati ya 12 wanaopanda jukwaani leo kuwania Taji lenye Sifa Kuu mbili ya Redd's Miss Sinza 2013, lakini pia linaloshikiliwa na Redd's Miss Tanzania 2012-2013, Brigit Alfred, leo katika Ukumbi wa Meeda Club uliopo Sinza Mori. Katika shindano hilo litakalosindikizwa na burudani kabambe kutoka kwa Bendi mahiri ya African Stars, 'Twanga Pepeta', viingilii vitakuwa ni Sh. 20,000/= kwa VIP na Sh. 10,000/= kwa viti vya kawaida. Shindano hili limedhaminiwa na Redds Original, Mtandao wa Sufianimafoto Blog, Dodoma Wine, Chilly Willy Energy Drink, Fredito Entertainment, CXC Africa, Clouds Media Group na Salut5.com. Picha na www.sufianimafoto.com
Mshiriki mwenye No, 9-SARAHY PAUL (23)..
Mshiriki mwenye No 8-HAPPYNESS MAIRA (19)
Mshiriki mwenye No, 11-NICOLE MICHAEL (21)
Mshiriki mwenye No, 5-PRISCA ELEMENT (20)
Mshiriki mwenye No, 3-MAUA ABDUL (18)
Mshiriki mwenye No, 7- AGNES SIMON (22)
Mshiriki mwenye No, 1-CATRINA LAURENCE (19)
 Mshiriki mwenye No, 6-JACQUELINE ROBERT (20)
 Mshiriki mwenye No, 4-DORIS MWAIPOPO (19) 

Mshiriki mwenye No, 10-MARTHA JOSEPH (19)
 Mshiriki mwenye No, 2-NASRA HASSAN (18)
 Mwalimu wa warembo hao, Mwajay Model, akionyesha uwezo wa kusebeneka, wakati akifungua rasmi shoo ya warembo hao ya kujitambulisha katika Promosheni maalum ya utambulisho wa shindano lao iliyoandaliwa na kinywaji cha Redd's katika Baa ya Mary Land Mwenge jijini Dar es Salaam, jana usiku. Kushoto ni mshereheshaji wa hafla hiyo fupi..... 

Warembo hao wakipozi kusubiri utaratibu baada ya kuwasili eneo la tukio jana usiku.

Warembo wakimshangilia mwenzao wakati akipita mbele kwenda kujitambulisha, ''sasa sijui na leo jioni huyu ndiye atakayeshangiliwa kama hivi?''

Mwalimu wa warembo hao, Majay (kulia) akipozi na warembo wake.

Hapa wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa mazoezi yao....ya maandalizi....

No comments:

Post a Comment