Friday, May 31, 2013

ZAMA ZA MOURINHO REAL MADRID KATIKA NAMBA


127 - Mourinho ameshinda mechi 127 kati ya 177 alizoiongoza klabu hiyo ya Real Madrid - jambo linalomaanisha kwamba ameshinda asilimia 72 ya mechi zote.

97 - Jumla ya mamilioni ya euro aliyoyatumia 'Spesho One' katika kusajili wachezaji wapya tangu alipotua miaka mitatu iliyopita.  

15 - Idadi ya mechi ambazo Mourinho aliwakabili Barcelona, ambapo alishinda NNE, alitoka sare TANO na kupoteza 'Clasico' SITA.

3 - Jumla ya mataji aliyoshinda Mreno huyo akiwa na Real Madrid katika miaka yake mitatu ya utawala wa Santiago Bernabeu. Alitwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Hispania (La Liga), Kombe la Mfalme na 'Ngao ya Jamii' (Spanish Supercup).

No comments:

Post a Comment