Friday, June 28, 2013

KANDA REDD'S MISS TANZANIA KUWAKA MOTO

Warembo wanaowania taji la Redd's Miss Temeke 2013 wakipiga picha ya pamoja baada ya mazoezi yao jijini Dar es Salaam leo

Warembo wanaowania taji la Redd's Miss Temeke 2013 wakipiga picha ya pamoja baada ya mazoezi yao jijini Dar es Salaam leo

KINYANG’ANYIRO cha kumpata Redd’s Miss Tanzania kwa mwaka huu kinazidi kushika kasi na sasa, kazi kubwa ipo katika ngazi ya kanda, ambapo leo atasakwa Redd’s Miss Kanda ya Mashariki na Redd’s Miss Kanda ya Ziwa.

Warembo wanaowania taji la Redds Miss Kanda ya Mashariki, watapanda jukwaani katika hoteli ya Nashera mjini Morogoro, kumsaka yule atakayefanikiwa kuondoka na taji hilo.

Wanne Star pamoja na wasanii wengine wa Morogoro ndiyo watakaonogesha shindano hilo, ambalo kiingilio chake kitakuwa Sh 10,000 kwa viti vya kawaida na Sh 20,000 viti maalumu.

Pia kazi nyingine kubwa ipo katika kumsaka Redd’s Miss Kanda ya Ziwa, shindano ambalo litafanyika katika ukumbi wa Nyerere ndani ya hoteli ya Gold Crest jijini Mwanza.

Katika shindano hilo, kutakuwa na burudani za kumwaga zitakazoongozwa na mkali wa Bongo Fleva, Ommy Dimpoz akishirikiana na Michael Ross na kiingilio kitakuwa Sh 20,000 viti vya kawaida na Sh 40,000 viti maalumu.

Shindano la Redd’s Miss Tanzania kwa sasa linadhaminiwa na kinywaji cha Redd’s Original kinachozalishwa na kusambazwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL).

No comments:

Post a Comment