Friday, June 28, 2013

NYOTA BONGO MOVIE KUMWAGA MISAADA

Nyota wa Bongo Movie, Snura (katikati) na Irene Uwoya (kulia) wakimuangalia mtoto aliyezaliwa wakati walipotembelea Hospitali ya Sekou Toure ya jijini Mwanza na kutoa msaada wa vyandarua wakati wa Tamasha la Filamu
Nyota wa Bongo Movie, Jacqueline Wolper akifunga chandarua wakati yeye na waigizaji wenzake walipotembelea Hospitali ya Sekou Toure ya jijini Mwanza na kutoa msaada wa vyandarua wakati wa Tamasha la Filamu

Kinamama wakiwa hosptalini wakati walipotembelewa na nyota wa Bongo Movie katika Hospitali ya Sekou Toure ya jijini Mwanza na kupokea msaada wa vyandarua wakati wa Tamasha la Filamu

Nyota wa Bongo Movie, Ray akikabidhi chandarua wakati yeye na waigizaji wenzake walipotembelea Hospitali ya Sekou Toure ya jijini Mwanza na kutoa msaada wa vyandarua wakati wa Tamasha la Filamu

WASANII mbalimbali watakaoshiriki katika Tamasha la Wazi la Filamu Tanzania, maarufu kama ‘Grand Malt Tanzania Open Film Festival’ ambalo litafanyika jijini Mwanza kuanzia keshokutwa, wanatarajia kutoa misaada mbalimbali kwa jamii.

Wasanii hao ambao wamewasili Mwanza leo, kesho wanatarajiwa kutembelea hospitali ya mkoa ya Sekou Toure, ambapo pia watatoa msaada wa vyandarua.

Mratibu wa tamasha hilo, Musa Kissoky, alisema wasanii hao watatoa msaada huo wa vyandarua, ikiwa ni mchango wao kwa jamii katika kupambana na malaria.

“Tayari wasanii karibu wote wameshawasili Mwanza, hivyo kesho wanatarajiwa kutembelea hospitali ya Sekou Toure na kutoa msaada wa vyandarua,” alisema.

Kuhusu maandalizi, Kissoky alisema, kwa sasa yamekamilika kwa asilimia 90, hivyo wakazi wa Mwanza wasubiri kuona vitu tofauti katika tamasha hilo.

Naye Meneja wa kinywaji cha Grand Malt walio wadhamini wakuu wa tamasha hilo, Consolata Adam, alisema wameamua kufanya kweli zaidi kwani wanataka kuona Watanzania wanapata kitu chenye uhakika.

“Tumejipanga katika hili na wala hatutanii kwani tunataka kuwawezesha wakazi wa Mwanza na maeneo ya jirani kuhudhuria tamasha hili kwa wingi.

“Tunawakaribisha watu wote wenye mapenzi na filamu zetu za Tanzania kufika na kushuhudia tamasha hili ambalo mwaka huu limeboreshwa zaidi,” alisema Consolata.

Tamasha hilo linatarajiwa kuanza Jumatatu ijayo, ambapo kutakuwa na maonyesho mbalimbali ya filamu pamoja na burudani za muziki kutoka bendi ya Extra Bongo, pamoja na ngoma za asili.

Tamasha hilo la filamu limedhaminiwa na kinywaji cha Grand Malt kisicho na kilevi ambacho kinazalishwa na kusambazwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL).

No comments:

Post a Comment