Friday, May 31, 2013

ABIDAL AMWAGA MACHOZI KUACHWA BARCELONA

Abidal akifuta machozi pembeni ya rais wa Barcelona Sandro Lopez wakati wa mkutano wao na waandishi wa habari kuhusu kuondoka kwa beki huyo.
Abidal (kulia) akiwa na Xavi katika basi la wazi wakati wakitembeza mitaani kombe lao la ubingwa wa La Liga msimu huu


RAIS Sandro Rosell alimsindikiza Eric Abidal katika mkutano na waandishi wa habari kufafanua sababu ya kumuacha aende:

"Yalikuwa ni maamuzi magumu sana kusema hapana kwa Abidal kutokana na heshima tuliyonayo kwake. Ingekuwa rahisi sana kusema ndiyo. Na unapokuwa unahisia za kweli naye, kama ilivyo kwangu, ugumu wake unakuwa ni mara tatu zaidi," alisema.

"Kwa sasa hatujaamua kuwanyang'anya jezi wachezaji. Heshima kubwa tunayoweza kumpa ni kuacha kuitumia namba yake uwanjani. Hatujafikiria kuhusu hilo, bado," rais huyo wa Barça alisema.

"Maamuzi yote yatachukuliwa kwa pamoja. Hayo ni maamuzi ya klabu," alisema.

"Abidal ametupa somo maishani ambalo hatuwezi kusahau. Daima atakuwa sehemu ya historia yetu. Tumeshea vipindi muhimu pamoja naye, furaha ya mataji, lakini mahusiano yetu yanaenda mabali zaidi ya kuwa rais – mchezaji. Hii si kwaheri, ila tutakutana tena.

"Milango ya Barça iko wazi kwake", aliongeza. "Siku yoyote akitaka kurejea, anaweza kurejea kama mkurugenzi wa soka wa timu ya vijana. Tutamsubiri hadi atakapoamua kustaafu kucheza soka. Kama atarejea na akaona anapenda kufanya jambo jingine, tutasikiliza anachosema. Asante, Eric. Ni jambo spesho sana kwangu kuwa nawe hapa leo. Najua hili si jambo rahisi kwako. Nakutakia mema," alikamilisha.

Kwa upande wake, mkurugenzi wa michezo, Andoni Zubizarreta alisema: "Ni maamuzi ambayo ukiyapokea inakuwa ngumu kupata usingizi."

Kila memba wa kikosi cha Barcelona alikusanyika pamoja kwa ajili ya kumuaga Eric Abidal, ambaye alikumbatiana na na wachezaji wenzake wa zamani kabla ya kuondoka kutoka kwenye chumba cha mkutano akionekana mwenye hisia sana.

No comments:

Post a Comment