Friday, May 3, 2013

REDD'S MISS KIBAHA KUTAMBULISHWA BILLICANAS MEI 8


WAREMBO wa Redds Miss Kibaha 2013, wanatarajia kuvamia Ukumbi wa kisasa wa burudani wa Club Billicanas, baada ya kualikwa kutembelea Jumatano ya Mei 8, lengo likiwa ni kujitambulisha kwa wadau wa sanaa ya urembo na burudani.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Linda Media Solution ambao ndio waandaaji wa shindano hilo, Khadija Kalili, alisema kuwa kutembelea klabu hiyo kutakuwa na faida kubwa kwa washiriki hao wa Miss Kibaha 2013.

Alisema wakati shindano lao likipangwa kufanyika Mei 17 mwaka huu mjini Kibaha, wanaamini washiriki wao watapata muda mzuri wa kukutana na watu wengi kwa pamoja, huku wakipita na kusalimia wadau wa sanaa nchini, wanaoingia katika klabu hiyo.

“Hii ni faida kwetu sisi kama waandaaji wa Miss Kibaha pamoja na mabinti wetu, ukizingatia kuwa tumepewa mwaliko huu wakati mzuri, hasa huu wa kujiandaa kwa vitu mbalimbali vyenye tija katika fainali zetu.

“Naamini kila jambo litafanyika kwa faida kubwa, huku washiriki wenyewe wakizidi kujipanga katika mazoezi yao ya kila siku yanayoendelea kufanyika kwa ajili ya kuhakikisha kuwa mambo yanakwenda vizuri,” alisema Kalili.

Miss Kibaha linadhamiwa na Redds Premium Clold, DSTV, Mama Kaka, Handeni Kwetu blog, Michuzi Blog, Jiachie Blog, Mtaa kwa Mtaa Blog, Maji Umoja, Shear Illusions, Fredito Entertainment, CXC Africa, Image Pub Temeke, Chicago Safari and Tours, ASET, Times FM, Clouds FM na Mikopo Finance.

No comments:

Post a Comment