Friday, May 3, 2013

MAMA WA CHRIS KELLY WA KRIS KROSS ALIYEFARIKI AWAAMBIA POLISI MWANAE ALIKULA COCAINE NA HEROIN

Marehemu Chris Kelly

DONNA Kelly Pratte, mama wa msanii Chris Kelly wa kundi la hip hop la Kris Kross, amewaambia maafisa wa polisi kwamba mwanae alianza kuugua baada ya kula dawa za kulevya aina ya cocaine na heroin usiku kuamkia siku aliyofariki.

Chris Kelly (34) alikutwa nyumbani kwake jioni akiwa hajitambui na akatangazwa kuwa amekufa katika hospitali ya Atlanta Medical Center, saa 11 jioni Jumatano.

Bado uchunguzi unaendelea kufahamu sababu halisi za kifo chake.

Tatizo pekee la kiafya alilokuwa nalo Kelly lilikuwa ni ugonjwa wa kunyonyoka nywele.


Chris Kelly akionekana na tatizo lake la kunyonyoka nywele

Chris Kelly akionekana na tatizo lake la kunyonyoka nywele

Tatizo la kunyonyoka nywele lilimsumbua tangu alipokuwa mdogo kama inavyoonekana kwa pembeni ya kichwa chake

'Alopecia Areata' ni ugonjwa nywele ambao unaathiri uotaji wa nywele za mwanadamu na ugonjwa huo ndiyo uliomuweka Kelly nje ya vyombo vya habari kwa zaidi ya miaka 10. Licha ya hali yake, Mac Daddy alikuwa bado na matumaini yote na katika mahojiano ya hivi karibuni alisema kwamba amerejea studio.

Kelly, aliyefahamika kwa jina la "Mac Daddy" alifanya kazi pamoja na Chris Smith, aliyefahamika kama "Daddy Mac," katika miaka ya mwanzoni mwa hadi katikati ya 90.

Kundi lao litakumbukwa zaidi kwa wimbo uliotamba wa "Jump" uliokuwa katika albam yao ya kwanza ya "Totally Krossed Out" ya mwaka 1992.


Februari mwaka huu Kris Kross waliungana pamoja kwa ajili ya tamasha la kusherehekea miaka 20 ya lebo ya So So Def ya Jermaine Dupri. Angalia video ya tamasha hilo chini:


No comments:

Post a Comment