Saturday, May 25, 2013

NEYMAR ASAINI MIAKA MITANO BARCELONA


 

Neymar akichuana na Messi wakati wa mechi yao ya fainali ya Kombe la Dunia la Klabu baina ya Barca na Santos mwaka juzi
Neymar akichuana na Glen Johnson wakati wa mechi baina ya timu ya taifa ya Brazil na England

Neymar (katikati) akikimbizwa na Gary Cahill (kulia) na Smalling (kushoto)

Neymar akionyeshana shughuli na Tom Cleverly
Karibu Barca mwana.... Neymar akipongezana na Lionel Messi baada ya mechi yao ya fainali ya Kombe la Dunia la Klabu mwaka juzi. 

BARCELONA imefanikisha kumsajili mshambuliaji wa Santos, Neymar kwa dau linalokadiriwa kuwa euro milioni 28 leo.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Brazil atajiunga na Barcelona kwa mkataba wa miaka mitano baada ya kukataa ushawishi wa Real Madrid, ambao wanaamini kwamba walitoa ofa nono ya euro milioni 35.

Mshambuliaji huyo ataingiza malipo binafsi ya euro milioni 7 kwa mwaka, ambayo licha ya kwamba ni pungufu ya ambayo angepata Real Madrid, yatamshuhudia akipata malipo ya ziada kutokana na maafikiano ya mkataba na kampuni ya kimataifa ya vifaa vya michezo ya Nike.

Neymar amekuwa katika rada za klabu nyingi kubwa za Ulaya kwa miaka kadhaa baada ya kung'aa Amerika Kusini na aliingia kuwania tuzo ya Ballon d'Or mwaka 2013.

Nyota huyo amekuwa akihusishwa na klabu kadhaa kubwa kama Chelsea, Bayern Munich na PSG, lakini Barcelona imeziacha mbali sana klabu hiyo kwa kupewa nafasi kubwa zaidi ya kumnasa nyota huyo mwenye umri wa miaka 21.

Mabingwa hao wapya wa La Liga, hata hivyo, wamewapiku mahasimu wao Real katika kumsajili Neymar ambaye atajiunga nao katika kipindi hiki cha usajili kujiandaa na msimu ujao wa 2013-14.

Kama sehemu ya dili hilo, Barcelona imeafiki kucheza mechi mbili za kirafiki dhidi ya Santos zenye thamani ya euro milioni 2 kila moja, hivi karibuni, moja kila bara - Amerika Kusini na Ulaya.

Klabuni Nou Camp, Mbrazil huyo atajiunga na nyota wenzake wanaotokea katika bara ya Amerika Kusini kama Lionel Messi, Alexis Sanchez, Javier Mascherano na nyota wenzake wa timu ya taifa ya Brazil, Dani Alves na Adriano.

Neymar alipata kusema siku za nyuma kwamba anataka kusubiri kuhamia Ulaya hadi baada ya fainali za Kombe la Dunia 2014, lakini kutokana na mkataba wake kumalizika mwakani, Santos wamelazimika kumuuza ili mchezaji huyo waliyemlea tangu mdogo asije kuondoka bure.  

No comments:

Post a Comment