Sunday, May 19, 2013

SH. MILIONI 500 ZAPATIKANA MECHI YA SIMBA, YANGA

Nahodha Nadir Haroub 'Cannavaro' akibeba taji la ubingwa wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya mechi yao waliyoshinda 2-0 dhidi ya Simba kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

MECHI ya watani wa jadi Simba na Yanga ya Ligi Kuu ya Vodacom iliyochezwa jana (Mei 18 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na kumalizika kwa mabingwa wapya Yanga kushinda mabao 2-0 yaliyofungwa na wachezaji wa kigeni Didier Kavumbagu na Hamisi Kiiza, imeingiza sh. 500,390,000.

Mechi hiyo namba 180 ambayo ilikuwa kati ya saba la kuhitimisha ligi hiyo msimu wa 2012/2013 ilishuhudiwa na watazamaji 57,406 waliokata tiketi kwa viingilio vya sh. 5,000, sh. 7,000, sh. 10,000, sh. 15,000, sh. 20,000 na sh. 30,000.

Kila klabu imepata mgawo wa sh. 123,970,927.45 wakati Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh. 76,330,677.97.

Kiingilio cha sh. 5,000 ndicho kilichovutia watazamaji wengi ambapo waliokata tiketi hizo walikuwa 19,039 na kuingiza sh. 95,195,000 wakati kile cha sh. 7,000 kiliingiza watazamaji 17,647 na kupatikana sh. 123,515,000.

Mgawo mwingine wa mapato hayo ni asilimia 15 ya uwanja sh. 63,036,064.81, tiketi sh. 3,818,890, gharama za mechi sh. 37,821,638.88, Kamati ya Ligi sh. 37,821,638.88, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 18,910,819.44 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 14,708,415.12.

No comments:

Post a Comment