Saturday, May 11, 2013

LAMPARD AVUNJA REKODI CHELSEA IKIFUZU MABINGWA ULAYA... SASA IMEBAKI NAFASI MOJA TU KWA ARSENAL AU SPURS

Shujaa wa rekodi... Frank Lampard akibebwa na kipa Petr Cech baada ya kumalizika kwa mechi dhidi ya Aston Villa kwenye Uwanja wa Villa Park mjini Birmingham, England leo. 
Lampard akishangilia baada ya kufunga goli lililoweka rekodi leo

Lampard akishangilia baada ya mechi dhidi ya Aston Villa leo

Lampard akifunga goli lake la kwanza katika mechi ya leo dhidi ya Villa

Lampard akishangilia baada ya kufunga huku akipongezwa na beki Ashley Cole

FRANK Lampard alifunga mara mbili na kuwa mchezaji wa Chelsea aliyeifungia timu hiyo mabao mengi zaidi katika historia yao wakati 'The Blues' walipozinduka kutoka nyuma na kushinda 2-1 ugenini dhidi ya timu iliyo katiika hatari ya kushuka daraja ya Aston Villa.

Christian Benteke aliwafungia Villa goli la kuongoza baada ya kukimbia kikamanda na kufunga bonge la goli, wakati Chelsea walijikuta wakibaki 10 baada ya Ramires kutolewa kwa kadi ya pili ya njano kabla ya mapumziko.

Baada ya mapumziko, Benteke naye alitolewa kwa njano ya pili na  Lampard akawasawazishia wageni.

Kiungo huyo kisha akafunga goli lake la 203 kwa Chelsea na kuivunja rekodi ya Bobby Tambling iliyodumu tangu mwaka 1970 na kuihakikishia Chelsea kucheza Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya msimu ujao.

Chelsea ni ya tatu katika msimamo huku ikiwa imebaki mechi moja na matokeo ya hesabu za miujiza pekee ndiyo yanayoweza kuwanyima nafasi ya kumaliza ndani ya Top 4.

Arsenal inaweza kumaliza juu ya Chelsea na Tottenham wanaweza kumaliza na pointi sawa nao, lakini tofauti ya magoli 17 waliyonayo Chelsea dhidi ya Spurs inamaanisha ni miujiza tu inayoweza kuwang'oa.

Ingawa matokeo hato yanawaacha Villa pointi tano juu ya ukanda wa kushuka daraja wakishika nafasi ya 13 katika msimamo, wamecheza mechi moja zaidi ya timu zote zilizo chini yao.

Bobby Tambling aliweka rekodi ya kufunga magoli 202 wakati alipoichezea Chelsea kuanzia mwaka 1959-70 wakati Lampard ambaye ni kiungo amefunga magoli 203 baada ya kuichezea klabu hiyo kwa misimu 12 yangu 2001.  

No comments:

Post a Comment