Thursday, May 16, 2013

BENITEZ APIGIWA MAKOFI ADIMU HATIMAYE

Rafa Benitez akibeba kombe la Ligi ya Europa jana
Ivanovic akishangilia juu ya lango
Kitoto cha Ramires kikitupia goli... kitoto hiki mashoto inaonekana kitakuja kuwa kama Mata

Ramires akikibusu kitoto chake

Ramires na mwanae

Shujaa... Torres akibeba kombe
John Terry akibeba vitoto vyake


AMSTERDAM, Uholanzi
RAFAEL Benitez aliandika historia nyingine katika utawala wake Jumatano, baada ya kuiongoza Chelsea kushinda 2-1 dhidi ya Benfica katika fainali ya Ligi ya Europa, kisha akaelezea namna ilivyokuwa kazi ngumu kufikia mafanikio hayo.

Kocha huyo Mhispania anaondoka baada ya kuongoza Chelsea kujihakikishia kucheza Ligi ya Klabu Bingwa msimu ujao na kuongeza kombe jingine katika kabati la mmiliki Roman Abramovich.

"Tumefunga magoli 145 na ni rekodi kwa klabu. Ni lazima ushinde kabla ya watu hawajaitambua kazi yake unayofanya. Hivyo tumeshinda, na watu wanaweza kusema 'ndiyo, hiyo ni nzuri'," aliwaambia waandishi wa habari.

Kocha huyo wa zamani wa Liverpool hakuwa chaguo linalopendwa na mashabiki katika kurithi mikoba ya kipenzi cha wengi Roberto Di Matteo, aliyefukuzwa Novemba mwaka jana licha ya kuiongoza timu hiyo kutwaa ubingwa wa Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya kwa mara ya kwanza katika historia miezi mitano iliyotangulia.

"Ni timu ambayo iko kwenye kipindi cha kukua ikiwa na wachezaji vijana hivyo ilikuwa ngumu sana tangu mwanzo. Nimefurahishwa sana na walichofanya licha ya kujua mwamba wako na kocha ambaye anaondoka mwisho wa msimu, bado walijituma kikamilifu," alisema.

Abramovich na bodi yake bado hawajateua kocha mpya, ingawa kocha wa Real Madrid, Jose Mourinho ambaye aliifungulia milango ya mataji Chelsea mwaka 2005, anaonekana kupewa nafasi kubwa ya kurejea.

Vyombo vya habari vya Uingereza na Hispania vimekuwa vikimhusisha Benitez na mipango ya kutua Everton na Malaga.
Mhispania huyo alipigiwa makofi adimu kutoka kwa mashabiki wa Chelsea mwisho wa mechi kwenye Uwanja wa Amsterdam Arena wakati alipojipanga kwa ajili ya kuipokea kombe pamoja na wachezaji wake.

Pamoja nao alikuwapo Fernando Torres, mshambuliaji wake wa zamani wa Liverpool ambaye alikuwa katika kiwango cha chini tangu aliposajiliwa Chelsea miaka miwili na nusu iliyopita lakini alifunga goli la kuongoza juzi baada ya kukimbia na mpira kutokea katikati ya uwanja kabla ya Branislav Ivanovic kufunga kwa kichwa katika dakika za lalasalama.

"Tuna wachezaji wengi ambao wanaongezeka ubora," Benitez alisema. "Fernando ni mmoja wao.

"Tumemtwaa ubingwa wa Ligi ya Europa tukiwa na mshambuliaji mmoja - mmoja tu. Tumeweza tukiwa na wachezaji wenye kadi za njano ... Unapochanganua unaona namna ilivyokuwa ngumu," aliongeza. "Na tulikuwa na wachezaji majeruhi ambao tumewakosa leo.

"Nadhani tumefanya vyema."

No comments:

Post a Comment