David Moyes, kocha mpya wa Man U |
Ferguson (kushoto) akiteta na kocha David Moyes |
David Moyes ndiyre atakayerithi mikoba ya Alex Ferguson katika kuiongoza Manchester United, klabu hiyo ya Ligi Kuu ya England imethibitisha leo (Alhamisi Mei 9, 2013) kupitia tovuti yake rasmi.
Kocha huyo wa Everton amekubali kuachana na klabu yake ya sasa kufikia mwishoni mwa msimu huu ili aanze rasmi kibarua chake kwenye klabu ya Man U kuanzia Julai Mosi na pia amekubali kusaini mkataba wa miaka sita kuifundisha Man U.
Ferguson mwenyewe alipendekeza kuwa Moyes ndiye awe mrithi wake kwa kusema: "Wakati tulipojadili kocha tunayedhani kwamba ana vigezo vinavyotakiwa wote tukamkubali David Moyes kwa kishindo. David ni mtu mwenye uadilifu mkubwa na pia mwenye kuzingatia miiko ya kazi. Nimekuwa nikivutiwa na uwezo wake kwa muda mrefu na niliwahi kumfuata kwa nia ya kutaka awe msaidizi wangu hapa tangu mwaka 1998".
"Wakati huo alikuwa bado kijana na ndiyo kwanza akianza kazi yake na tangu wakati huo amefamnyua kazi kubwa ya kuisuka Everton. Hakuna swali kuhusiana na ukweli kwamba ana vigezo vyote tunavyovitarajia kutoka kwa kocha wa kuiongoza klabu hii".
Moyes, ambaye amekuwa akiifundisha Everton kwa miaka 11 sasa, ameungwa mkono pia na Bobby Charlton, mmoja wa magwiji wa Man U.
No comments:
Post a Comment