Thursday, May 16, 2013

LAMPARD ASAINI MKATABA MPYA MWAKA MMOJA CHELSEA

Lampard (katikati) akibeba kombe pamoja na wenzake
Mabingwa wakifurahi baada ya kukabidhiwa kombe

LONDON, England
MFUNGAJI anayeshikilia rekodi ya kufunga magoli mengi zaidi wa Chelsea, Frank Lampard amesaini mkataba wa mwaka mmoja na mabingwa hao wa Ligi ya Europa, klabu hiyo ya Ligi Kuu ya England imesema leo.

Kiungo huyo wa England mwenye umri wa miaka 34, ambaye alivunja rekodi ya muda wote ya Chelsea iliyokuwa ikishikiliwa na Bobby Tambling ya kufunga magoli 202 mwezi huu, sasa atabaki Stamford Bridge kwa msimu wake wa 13.

"Tulikujwa tukizungumza naye tangu mwisho wa mwaka jana na mazungumzo yetu yamekuwa chanya kwa wakati wote. Tuna furaha kutangaza sasa kwamba tumemuongeza mkataba utakaomweka klabuni hadi 2014," mkurugenzi mtendaji Ron Gourlay aliiambia tovuti ya klabu hiyo (www.chelseafc.com).

Lampard alisema amefurahishwa: "Kila mtu anafahamu kwamba daima nilidumisha ndoto yangu ya kubaki Chelsea. Tumekuwa tukizungumza kwa muda mrefu na daima imekuwa ikienda vyema.
"Kuisaidia klabu kupata mafanikio katika miaka ijayo ndicho kitu pekee ambacho nimekuwa nikikihitaji. Nina furaha sana."

No comments:

Post a Comment