Monday, April 1, 2013

TAZAMA ZOEZI LA MWISHO LA KUNASUA MAITI KATIKA JENGO LA GHOROFA 16 LILILOPOROMOKA IJUMAA JIJINI DAR ES SALAAM... MAITI ZILIZOPATIKANA SASA ZAFIKIA 36... RAIS JK ASHUKURU WANAJESHI NA WOTE WALIOSHIRIKI UOKOAJI

Zoezi la kuondoa kifusi katika sehemu ya chini kabisa ya jengo lililoporomoka la ghorofa 16 likiendelea kukamilishwa leo April 1, 2013.
Duh... eti hili ndilo eneo lililokuwa na msingi wa jengo la ghorofa 16 kabla ya kuporomoka Ijumaa wakati likiendelea kujengwa katika makutano ya Morogoro Road na Indira Gandhi jijini Dar es Salaam... uokoaji umekamilishwa leo April 1, 2013.
Timu ya waokoaji yenye wataalam mbalimbali ikiendelea kukamilisha kazi leo April 16, 2013. 
Kama siamini vile..! Hapa ndipo liliposimama jengo la ghorofa 16 lililoporomoka Ijumaa na kuua watu 36 huku wengine kibao wakijeruhiwa.
Waokoaji wakiendelea kukamilisha kazi yao leo April Mosi, 2013.
Askari wa JKT walikuwa bega kwa bega hadi mwisho... hapa wakisaka watu zaidi kwenye eneo la chini kabisa (basement) leo April Mosi, 2013.
Nd'o hapa paliposimama mjengo wa ghorofa 16... waokoaji wakiendelea kukamilisha kazi leo April 1, 2013.
Hakuna mwili wa mtu mwingine?
Haikuwa kazi ndogo mzee... kamanda mmoja wa JWTZ akimfafanulia jambo mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Said Mecky Sadick aliyetembelea eneo la ajali wakati wa kukamilisha kazi ya uokoaji baada ya kufikiwa kwa jengo la chini kabisa lililobeba maghoroga 16 ya mjengo ulioanguka Ijumaa na kuua watu 36. Hapa ni leo April 1, 2013.
Tumemaliza kazi mzee...!
Miili ya watu walionasuliwa kutoka katika kifusi cha jengo la ghorofa 16 lililoporomoka Ijumaa asubuhi wakati likiendelea kujengwa kwenye makutano ya Morogoro Road na Indira Gandhi jijini Dar es Salaam sasa imeongezeka na kufikia 36.

Idadi hiyo inatokana na miili mengine saba kupatikana hadi kufikia leo wakati zoezi la uokoaji na kunasua miili ya watu waliofukiwa na vifusi vya jengo hilo kuelekea kukamilika baada ya leo (Aprili Mosi, 3013) vikosi vya uokoaji kufikia jengo la chini kabisa (basement).

Jengo hilo lililokuwa likiendelea kujengwa, liliporomoka Ijumaa katika siku iliyokuwa ya mapumziko ya 'Ijumaa Kuu', mishale ya saa 2:30 asubuhi.
 
Rais Jakaya Kikwete, ambaye alitembelea eneo la tukio masaa machache tu baada ya kutokea, aliagiza kwamba wahusika wote waliosababisha maafa hayo wafikishwe mbele ya mkono wa sheria na hadi sasa, polisi wamesema kuwa tayari wameshawatia mbaroni watuhumiwa wanne.

Katika hotuba yake ya kila mwezi jana, Rais Kikwete alisema amehuzunishwa sana na tukio hilo la kuanguka kwa jengo hilo lakini ameridhishwa na juhudi kubwa za uokoaji zilizofanywa na wanajeshi wakishirikiana na taasisi, mashirika binafsi na wananchi wa kawaida.

“Napenda kutumia nafasi hii kutoa shukrani maalum kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Saidi Meck Sadick kwa uongozi wake madhubuti.  Pia nampongeza Mkuu wa Wilaya ya Ilala,  Raymond Mushi, na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam,  Suleiman Kova pamoja na maafisa na askari wa JWTZ, na wale wote walioshiriki na wanaoendelea kushiriki katika juhudi za uokoaji,” alisema. 

Rais Kikwete aliwapa pole wale wote waliofiwa na akaagiza watakaothibitika kusababisha maafa hayo wachukuliwe hatua zinazostahili, ikiwa ni pamoja na kuwaburuza mahakamani na wengine kufutiwa leseni za kufanya shughuli za ujenzi.

No comments:

Post a Comment