Monday, April 1, 2013

PROFESA JAY AFUNIKA TAMASHA LA VODACOM COCO BEACH

Fid Q akipagawisha mashabiki Coco Beach wakati wa Tamasha la Vodacom jana.

Prof Jizzle akiwaimbisha mashabiki wakati akitumbuiza jana

Fid Q akipanda stejini Coco Beach wakati wa Tamasha la Vodacom jana.

Stamina akipiga michano wakati wa tamasha hilo

NYOTA wa muziki wa hip hop nchini, Joseph Haule a.k.a Profesa Jay, aliacha gumzo wakati alipofanya shoo uhakika katika tamasha la wazi lililoandaliwa na kampuni ya huduma za simu ya Vodacom Tanzania kwenye Ufukwe wa Coco jijini Dar es Salaam jana.

Wasanii wengine waliofanya vyema katika tamasha hilo lililohudhuriwa na watu wengi walikuwa ni Stamina na Fid Q.

Tamasha hilo lililofanyika maalum katika Sikukuu ya Pasaka, liliandaliwa maalum na Vodacom kwa ajili ya kusherehekea na wateja wao, pamoja na kuelimishwa kuhusu huduma mbalimbali zinazotolewa na kampuni ya hiyo.

Akizungumza katika tamasha hilo, Afisa Udhamini na Matukio wa Vodacom Tanzania, Ibrahim Kaude, aliwashukuru Watanzania kwenda kwa wingi katika tamasha hilo la bure na kushiriki pamoja katika tukio hilo la kiburudani.

Alisema kuwa katika tamasha hilo, wateja wao walikuwa wakipewa elimu jinsi mtandao wao unavyofanya kazi, ikiwapo kujulishwa huduma mbalimbali zinazotolewa na kampuni hiyo.

Profesa Jay alikuwa wa kwanza kupanda jukwaani kutoa burudani na kuungwa mkono wakati akiwaimbisha mashabiki walioonekana kupagawa.

Rapa huyo veterani, alifuatiwa na Stamina ambapo dakika kumi baadaye, Fid Q naye alipanda na kufanya shoo pamoja na mkali huyo wa hip hop anayekubalika na watu wengi kutokana na nyimbo zake kali ukiwamo wa 'Kabwela'.

Tamasha la wazi la Vodacom lililofanyika kwa siku mbili katika ufukwe huo wa Coco.

No comments:

Post a Comment