Gerard Pique (kulia) na Victor Valdes wakiwa wameloa baada ya kupigwa 4-0 dhidi ya Bayern Munich |
MIAKA mitano baada ya Barcelona kuinyanyasa dunia kwa mara ya kwanza kutokana na soka lake la pasi nyingi, huu hapa ni uchambuzi wa sababu zilizoifanya timu hiyo kusambaratika katika mechi dhidi ya Bayern Munich.
1. Wachezaji hawapumzishwi
Wachezaji wa Barcelona wanaonekana kuchoka kuelekea mwisho wa msimu kwa sababu hawakuwa wakipumzishwa vyema na kuwapisha wengine kikosini.
2. Tito Vilanova hawaamini wachezaji wake wa akiba
"Sub" moja tu ilifanyika dhidi ya Bayern - tena katika dakika ya 83 katika mechi ngumu ambayo walilala 4-0.
3. Benchi la ufundi limelala
Mambo yalipokuwa yakielekea kuwa mabaya benchi la ufundi halikufanya chochote kuokoa hali ya mambo.
4. Usajili mbovu na hawakuitumia fursa ya dirisha dogo
Alex Song alisajiliwa, lakini ameshindwa kuwa na mchango.
Lionel Messi |
5. Hamna "Plan B" baada ya Messi
Wengi wanaamini kwamba timu inamtegemea kwa kila kitu Lionel Messi.
6. Hakuna kilichofanywa kuziba maeneo dhaifu ya msimu uliopita
Bodi ya wakurugenzi na benchi la ufundi waliamua kubaki na wachezaji wao walewale. Guardiola alibaini matatizo yaliyohitaji kurekebishwa - Dani Alves alikuwa mmojawapo.
7. Majeraha na kuugua
Kumekuwa na majeruhi wa muda mrefu - yakiwamo yale yaliyomkuta Javier Mascherano na Carles Puyol. Adriano, Alexis Sanchez na Cesc Fabregas wote walitumia sehemu kubwa ya msimu wakiwa nje kutokana na majeraha na kuugua. Kisha kuna Eric Abidal na kocha Tito Vilanova.
8. Kukosa ungangari na umakini uwanjani
Udhaifu wa timu katika ulinzi katika ligi umekuwa ni tatizo kubwa dhidi ya timu kubwa za Ulaya.
9. Mabadiliko ya staili
Moja ya staili ya timu ilikuwa ni kuwanyima pumzi wapinzani kwa kuwafanya "wausake mpira kwa tochi" na kuwapiga presha kubwa ya kuwabana wanapokuwa na mpira. Staili ya timu sasa ni kushambulia zaidi.
10. Hatma ya Victor Valdes
Victor Valdes ametangaza hadharani kwamba hatabaki klabuni hapo mkataba wake utakapomalizika 2014. Tangazo hilo limekitikisa kikosi.
No comments:
Post a Comment