Saturday, March 9, 2013

UHURU KENYATTA AWA RAIS MPYA WA KENYA... AFIKISHA ASILIMIA 50 YA KURA KWA KUMGARAGAZA VIBAYA HASIMU WAKE RAILA ODINGA ALIYEMUACHA KWA TOFAUTI YA KURA 832,887... NI BAADA YA MATOKEO YA MAJIMBO YOTE 291 KUTANGAZWA...!

Rais mpya wa Kenya, Uhuru Jomo Kenyatta
Weweeeeee...! Baadhi ya wananachi wakifurahia ushindi wa Uhuru kwenye Barabara ya Thika usiku wa kuamkia leo.

Uhuru nomaaaa...! Wananchi wa Kenya katika wakifurahia ushindiwa Uhuru katika mitaa ya jiji la Nairobi usiku wa kuamkia leo.
Unachukua, unaweka... waaaaaaaa! Wafuasi wa Uhuru wakifurahia ushindi jijini Nairobi usiku wa kuamkia leo Machi 9, 2013.
Uhuru akinadi sera zake wakati wa kampeni


 Uhuru Kenyatta ambaye alikuwa akigombea urais wa Kenya kwa tiketi ya chama cha The National Alliance (TNA) ameibuka kidedea baada ya kuzoa kura 6,173,433 dhidi ya hasimu wake Raila Odinga wa chama cha Cord aliyeambulia kura 5, 340,546.

Kwa idadi ya kura hizo kutoka katika majimbo yote 291, Uhuru ambaye ni mtoto wa rais wa kwanza wa Kenya, marehemu Jomo Kenyatta, amemuacha Odinga kwa kura 832,887 na pia amevuka asilimia 50 ya kura zote kwani kimahesabu amepata
asilimia 50.7 kati ya kura 12,338, 667 zilizopigwa; hivyo kukidhi vigezo vya kutangazwa kuwa mrithi wa rais anayemaliza muda wake, Mwai Kibaki. Katiba mpya ya Kenya inataka mshindi ni lazima afikishe asilimia 50 na kama hakuna mgombea anayepata kura za idadi hiyo, uchaguzi hurudiwa kwa mara ya pili na kuwahusisha vinara wawili. 

Kura zilizoharibika kutoka katika majimbo yote ni 108,975 na kura halali zilizomuibua mshindi ni 12,222,980.

Wanaowafuatia Uhuru na Odinga ni Musalia Mudavadi aliyepata 483,981, Peter Kenneth (72,786), mgombea wa Alliance for Real Change, Mohamed Abduba Dida (52,848), Martha Karua wa National Rainbow Coalition (43,881), James Ole Kiyiapi wa Restore and Build Kenya (40,998) na wa mwisho miongoni mwawagombea nane walioshiriki kinyang'anyiro hicho ni Paul Kibugi Muite kutoka chama cha Safina.

Uhuru aliyeshinda safari hii baada ya kuungwa mkono na muungano wa Jubilee, aligombea urais kwa mara ya kwanza miaka 10 iliyopita na kugaragazwa na muungano wa kina Mwai Kibaki na Raila Odinga.


 Wakati wa uchaguzi wa mwaka 2007, Uhuru hakugombea na badala yake alimuunga mkono Mwai Kibaki kupitia muungano wao uliounda chama cha PNU.

No comments:

Post a Comment