Friday, March 8, 2013

DRAKE AMWAGA SAKAFUNI MILIONI 80/- KWENYE KLABU YA VIMWANA WANAONENGUA BILA NGUO

Drake akimwaga pesa kwenye klabu ya usiku

PESA si chochote kwa Drake. Rapa huyo bilionea wa lebo ya kurekodi muziki ya Young Money alifika katika klabu ya usiku mjini Charlotte, North Carolina, na kumwaga mvua ya pesa — zenye thamani ya dola 50,000 (sawa na zaidi ya Sh. milioni 80).

Wakati akiwa katika klabu hiyo ya usiku iitwayo Cameo, alifungua boksi na kutawanya pesa akizirusha hewani na kuzishuhudia zikitua sakafuni kama mvua.

Tovuti ya TMZ ilipata picha zinazomuonyesha Drizzy akifanya tukio hilo akiwa pamoja na wapambe wake.

Madansa ambao hunengua bila ya nguo katika klabu hiyo ya usiku walionekana kupagawa kwenye mvua ya noti zenye thamani ya Sh. milioni 80. Kulikuwa na noti nyingi sana zimezahaa sakafuni.

Angalia picha za Drake akimwaga utajiri.No comments:

Post a Comment