Pole shosti... ndiyo mipango ya Mungu! Wema (kulia) akimfariji Kajala. |
Haa haa haaaa haaaa... Wema akifurahia na Kajala baada ya kufanikiwa kumchomoa lupango kwa kulipa mkwanja alioamuru pilato wa 'em 13' taslim! Chezea Wema weye! |
Kicheko cha furaha... |
Pole sana mamaa... Msanii Dk. Cheni akimfariji Kajala |
Mama yake Lulu aitwaye Lucrecia Karugila (kushoto) akiongoza kikao kidoooogo nje ya mahakama ya Kisutu kuhusiana na namna ya kumchomoa Kajala |
Dah... yaani mamwela swalishamswaga Kajala kwenye karandinga kuanza safari kwenda lupango. Wema alicheza kama Pele kwenda kuwahi kulipa faini na kumuokoa asiende jela...! |
Tutamtoaje? Lulu na shosti yake mmoja wakijadili namna ya kumchomoa Kajala |
Hapa ni wakati akipelekwa kwa pilato kusomewa hukumu |
Akielekea kwenye karandinga kabla ya Wema kumchomoa |
Sijui itakuwaje? Hapa ni kabla Wema hajafanya makaratee yake na kumchomoa... karandinga lilishakuwa tayari kumbeba na kumpeleka lupango chini ya ulinzi mkali wa 'mamwela' wa Magereza |
Mume wa Kajala
aitwaye Faraja Chambo, pia alikumbana na adhabu ya kifungo cha kwenda jela
miaka 12 au kulipa faini ya Sh. milioni 213 baada ya kukutwa na hatia kutokana
na makosa hayo na jingine la tatu la utakatishaji fedha.
Hukumu hiyo
ilitolewa jana na Hakimu Mkazi Sundi Fimbo wa Mahakama ya Kisutu.
Hata hivyo,
wakati mumewe Chambo akipelekwa gerezani baada ya kushindwa sharti la kulipa
faini, Kajala aliachiwa huru saa chache baadaye kufuatia msanii mwenzake nyota
wa filamu nchini, Wema Sepetu kuwahi kwenda benki na kurejea mahakamani kumlipia
faini (Sh. milioni 13).
Mwishowe, baada
ya kukamilisha taratibu zote mahakamani hapo, Kajala akaachiwa huru saa 7:37
mchana na kulakiwa na ndugu, jamaa na marafiki waliojazana tele kujua hatma
yake; baadhi yao wakiwa ni wasanii Elizabeth Michael Michael 'Lulu', Muhsen
Awadh "Dk. Cheni' . Miongoni mwao alikuwapo pia mama yake Lulu, Lucresia
Karugila.
KESI YENYEWE
Awali, wakati
Hakimu Fimbo akisoma hukumu ya kesi hiyo kuanzia saa 4:33 hadi saa 5:49
asuhuhi, Kajala alionekana kizimbani akibubujikwa machozi muda wote.
Akisoma hukumu
hiyo, Hakimu Fimbo alisema baada ya kupitia ushahidi uliotolewa na pande zote
mbili, mahakama imewatia hatiani washtakiwa wote wawili kwa makosa mawili
ambayo ni pamoja na kula njama ya kuhamisha umiliki wa nyumba iliyopo Kunduchi
Salasala jijini Dar es Salaam.
Washtakiwa hao,
pia kwa pamoja walikutwa na hatia ya shtaka la pili la kuhamisha isivyo halali
umiliki wa nyumba hiyo kwenda kwa Emiliana Rwegarura huku wakijua kwamba
imepatikana kwa njia ya rushwa.
"Siuo kweli
kama washtakiwa hawakujua kuwa kuna hati ya kuzuia nyumba hiyo kuuzwa... lakini
waliidharau hati hiyo na kuiuza nyumba hiyo kinyume cha sheria," alisema
Hakimu Fimbo.
"Mshtakiwa
wa kwanza (mume wa Kajala) amekutwa na hatia pia katika shtaka la tatu kwa
sababu ushahidi umeonyesha kuwa alizipata fedha hizo kwa njia ya utakatishaji
haramu na Kajala ameachiwa huru kwavile hakujua fedha hizo zilipatikana vipi...
lakini alihusika katika kuuza nyumba hiyo," alisema Hakimu Fimbo.
Kabla ya kusomwa
adhabu ya washtakiwa hao, Mwendesha Mashtaka wa Takukuru, Leonard Swai,
aliiomba mahakama kutoa adhabu kali kwa washtakiwa ili iwe fundisho kwa watu
wenye tabia kama ya washtakiwa.
Katika kesi
hiyo, washtakiwa walikuwa wanakabiliwa na mashtaka matatu, likiwamo la kuhamisha umiliki, kula njama kinyume cha
kifungu cha 34 cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa ya mwaka 2007 huku
wakijua ni kosa kwani tayari Mwanasheria Mkuu wa serikali alishazuia uuzwaji wa
nyumba hiyo.
Katika shtaka la
pili, ilidaiwa kuwa Aprili 14 mwaka 2010, washtakiwa hao walihamisha isivyo
halali umiliki wa nyumba hiyo kwenda kwa Emiliana Rwegarura huku wakijua imepatikana
kwa njia ya rushwa, kinyume cha kifungu cha 34(2)A(3) cha Sheria ya Kuzuia na
Kupambana na Rushwa ya mwaka 2007.
Katika shtaka la
tatu, ilidaiwa kuwa siku na mahali hapo washitakiwa hao walitakatisha fedha huku
wakijiua ni kinyume na sheria hiyo.
Awali, kwa
nyakati tofauti, washtakiwa walikana mashtaka yote lakini kwavile mashtaka hayo
hayana dhamana kisheria, wote wawili walikuwa mahabusu hadi jana ilipotolewa
hukumu.
No comments:
Post a Comment