Tuesday, March 26, 2013

VILANOVA ARUDI BARCELONA AKITOKEA MAREKANI LEO... AREJEA AKIWA NA SHAVU NEEEENE BAADA YA KUPATA NAFUU KUFUATIA TIBA YA KANSA YA KOO ILIYOCHUKUA MIEZI MIWILI

Vilanova akwiasili Barca leo huku akionekana kuwa na shavu dodo.
BARCELONA, Hispania
Kocha wa Barcelona, Tito Vilanova amerejea leo nyumbani kwao mjini Barcelona na atapumzika kwa muda kabla ya kuanza kurejea polepole katika kazi yake.

Vilanova amerejea kwao Hispania akitokea Marekani alikokaa kwa miezi miwili akitibiwa kansa ya koo, klabu yake inayoshiriki La Liga, Ligi Kuu ya Hispania ilisema katika taarifa yake jana.

Vilanova aliwasili Barcelona mapema leo na kuonekana akiwa na shavu 'dodo' , kisha baadaye akaenda kupumzika nyumbani kwake.

No comments:

Post a Comment