Thursday, March 21, 2013

BARCELONA, MESSI NA INIESTA WAKOMBA TUZO LEO KUTOKA KWA SHIRIKISHO LA KIMATAIFA LA HISTORIA NA TAKWIMU ZA SOKA(IFFHS)

Messi na tuzo za IFHHS leo
BARCELONA, Hispania
Shirikisho la Kimataifa la Historia na Takwimu za Soka (IFFHS) limeitangaza klabu ya Barcelona kuwa ndiyo timu bora Duniani kwa mwaka 2012

Tuzo waliyotwaa Barcelona leo ni ya nne, na pia ni ya mara ya tatu katika kipindi cha miaka minne iliyopita.

Lionel Messi na Andres Iniesta wametangazwa pia na IFFHS kuwa ndiyo washindi wa tuzo za mfungaji bora Duniani (Messi) na kiungo mchezeshaji bora Duniani (Iniesta).

Iniesta ametangazwa kuwa mshindi wa tuzo ya Kiungo Mchezeshaji Bora wa Dunia mwaka 2012, ambayo awali ilishatwaliwa mara nne na swahiba wake Xavi Hernández wa Barcelona.

Lionel Messi ametangazwa na IFFHS kuwa mshindi wa tuzo ya Mfungaji Bora Duniani mwaka 2012, kwake ikiwa ni mara ya pili mfululizo.

No comments:

Post a Comment