Sunday, March 31, 2013

MAN UNITED YAMFUKUZISHA KAZI KOCHA SUNDERLAND

Martin O'Neill

Pole mtu mzima... Kocha Sir Alex Ferguson akizungumza na Martin O'Neill kabla ya mechi baina ya Sunderland na Manchester United kwenye Uwanja wa Stadium of Light mjini Sunderland, England jana. Man Utd ilishinda 1-0.

KLABU iliyo katika hatari ya kushuka daraja ya Sunderland imemfukuza kocha Martin O'Neill kufuatia matokeo mabaya.

Sunderland wako pointi moja tu juu ya ukanda wa kushuka daraja zikiwa zimebaki mechi saba baada ya kipigo cha 1-0 kutoka kwa Manchester United jana.

Sunderland hawajashinda hata mechi moja kati ya nane zilizopita, ambapo wameambulia pointi tatu tu.

Klabu hiyo imesema maamuzi ya kumpata mrithi wa O'Neill "yatafanywa katika siku zijazo."

Kocha huyo raia wa Ireland Kaskazini alichukua kiti hicho kutoka kwa Steve Bruce miezi 16 iliyopita, akaiongoza Sunderland kushinda mechi saba katika 10 za kwanza na kuipunguzia hofu ya kushuka daraja ambapo walipaa hadi nafasi ya 13 katika msimamo.

O'Neill (61) ambaye pia amewahi kuzifundisha klabu za Wycombe, Norwich, Leicester, Celtic na Aston Villa alionekana kuiimarisha timu wakati alipomsajili winga wa England, Adam Johnson na mshambuliaji wa Scotland, Steven Fletcher mwisho wa msimu uliopita.

Matokeo yaligoma hata hivyo, na Sunderland ikaangukia nafasi ya 16 katika msimamo kufuatia kipigo chao cha jana ambacho kilitokea bila ya kuwapo kwa kinara wao wa mabao Fletcher na nahodha Lee Cattermole baada ya majeruhi hao wawili kuambiwa kuwa watakuwa nje msimu mzima.

O'Neill anaondoka Sunderland akiwa na rekodi ya kushinda mechi 16 kati ya mechi 55 za Ligi Kuu ya England.

No comments:

Post a Comment