Sunday, March 31, 2013

MESSI AZIDI KUWEKA MAREKODI... AZITUNGUA TIMU PINZANI ZOTE 19 MFULULIZO LA LIGA

Lionel Messi wa FC Barcelona akishangilia baada ya kufunga dhidi ya RC Celta de Vigo kwenye Uwanja wa Estadio Balaidos mjini Vigo, Hispania jana usiku Machi 30, 2013. Timu hizo zilitoka 2-2.

Lionel Messi (kulia) wa FC Barcelona akishangilia pamoja Cristian Tello baada ya kufunga dhidi ya RC Celta de Vigo kwenye Uwanja wa Estadio Balaidos mjini Vigo, Hispania jana usiku Machi 30, 2013. Timu hizo zilitoka 2-2.
Lionel Messi (10) wa FC Barcelona akishangilia pamoja na wenzake baada ya kufunga dhidi ya RC Celta de Vigo kwenye Uwanja wa Estadio Balaidos mjini Vigo, Hispania jana usiku Machi 30, 2013. Timu hizo zilitoka 2-2.

Cristiano Ronaldo wa Real Madrid CF akipongezwa na Marcelo baada ya kufunga goli la kusawazisha dhidi ya Real Zaragoza kwenye Uwanja wa La Romareda mjini Zaragoza, Hispania Machi 30, 2013. Timu hizo zilitoka 1-1.

Cristiano Ronaldo wa Real Madrid CF akikimbia kwenda kufunga goli la kusawazisha dhidi ya Real Zaragoza kwenye Uwanja wa La Romareda mjini Zaragoza Hispania Machi 30, 2013. Timu hizo zilitoka 1-1.

Cristiano Ronaldo (7) wa Real Madrid akipongezwa na Kaka (kushoto), Luka Modric (wa pili kushoto) baada ya kufunga goli la kusawazisha dhidi ya Real Zaragoza kwenye Uwanja wa La Romareda mjini Zaragoza Hispania Machi 30, 2013. Timu hizo zilitoka 1-1.

MSHAMBULIAJI wa Barcelona, Lionel Messi amekuwa mchezaji wa kwanza katika historia ya soka la Hispania kufunga dhidi ya kila timu katika mechi za La Liga mfululizo.

Mwanasoka bora wa dunia mara nne mfululizo Messi alifunga katika mechi yake ya 19 mfululizo wakati Barca iliposhikiliwa katika sare ya 2-2 ugenini dhidi ya Celta Vigo jana usiku na hivyo kuwa amezifunga timu zote 19 pinzani mfululizo katika ligi hiyo ya timu 20.

Messi amepachika juma la magoli 30 katika mechi hizo 19 na hivyo kufikisha jumla ya magoli 43 katika La Liga msimu huu. Katika michuano yote msimu huu amefunga juma la magoli 56.

Barca wako kileleni kwa tofauti ya pointi 13 juu ya Real Madrid, walio katika nafasi ya pili huku zikiwa zimesalia mechi tisa.

Mabingwa watetezi, Real nao walidondosha pointi jana baada ya kushikiliwa katika sare ya 1-1 dhidi ya Zaragoza. Cristiano Ronaldo alifunga goli lake la 113 katika mechi 100 akiwa na miamba hao wa Hispania chini ya kocha Jose Mourinho.

Lionel Messi ndiye kinara wa mabao katika ligi tano kubwa za Ulaya kwa mwaka 2013 (kuanzia Januari 1, 2013) akiwa amefunga mabao 17 ya ligi. Cristiano Ronaldo amefunga mabao 14 ya ligi na Robert Lewandowski 10.

Mjini Vigo, Messi alivaa kitambaa cha unahodha jana na akaendelea kuimarisha rekodi yake ya awali ya kufunga mfululizo.

Rekodi iliyowekwa kabla yake katika La Liga, ilikuwa ni ya kufunga magoli katika mechi 10 mfululizo na iliwekwa na Ronaldo de Lima.

Barca walitanguliwa kufungwa na Natxo Insa lakini Messi akampikia
Cristian Tello goli la kusawazisha kisha Tello akarejesha fadhila kwa kumpikia Mess bao la pili kabla ya wenyeji kusawazisha katika dakika ya 88 kupitia kwa Borja Oubina.

Barca sasa inasafiri kwenda Ufaransa kwa ajili ya mechi yao ya kwanza ya robo fainali ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya dhidi ya Paris Saint-Germain keshokutwa.

----------

No comments:

Post a Comment