Thursday, March 7, 2013

LIONEL MESSI ASEMA MILAN LAZIMA WANG'OKE NOU CAMP... ASIFU KIWANGO CHA REAL MADRID DHIDI YA MAN U LAKINI AKATAA KUJILINGANISHA NA CRISTIANO RONALDO KWA KUSEMA: "HATUCHEZI ILI KUANGALIA NANI MKALI KATI YETU... WANAOLINGANISHA NI WAANDISHI WA HABARI..!

Lionel Messi
BARCELONA, Hispania
Straika Lionel Messi amezungumza na vyombo vya habari kuelezea hali ya sasa inayoikabili klabu yake ya Barcelona huku akisem: "Tumeumizwa na vipigo vya hivi karibuni, lakini tutaondokana na hali hii.

"Mimi sijahuzunishwa, sijui ni nani aliyesema hayo," ameongeza Messi huku usoni akionekana kuchanganywa na taarifa hiyo.

"Kiasi tunapaswa kujituma zaidi. Tumeshajua kabisa matatizo yalikuwa wapi, lakini hilo linabaki kuwa siri yetu ndani ya vyumba vya kubadilishia nguo," amesema Messi, ambaye hivi sasa anaangalia zaidi mechi yao ya wiki9 ijayo dhidi ya Milan:"Natumai tutabadili matokeo na kurejea katika kasi yetu dhidi ya Milan. Kama wao walivyoshinda kwao (2-0), na sisi tunaweza kushinda hapa Barcelona. Sote tunajua kwamba kiasi tunapaswa kujituma zaidi. Tuna mechi muhimu inayokuja kubadili hali ya mambo."

Messi aliongeza, "Kilichowatokea Tito na Abidal (waliokumbana na maradhi na kufanyiwa upasuaji) kimetuathiri. Lakini hatuwezi kulalamikia hali hiyo. Tuna kikosi imara na hivyo tutajirekebisha."

Akibadili mjadala huo, Messi alizungumzia kuimarika hivi karibuni kwa kiwango cha mahsimu wao wa jadi, Real Madrid na nyota mwenzake Cristiano Ronaldo: "Niliitazama mechi ya Real Madrid (dhidi ya Man U). Ilithibitisha ni kwa namna gani walivyokuwa na timu imara. Timu yoyote ambayo ingefuzu miongoni mwa hizo mbili ina nafasi ya kuwa moja ya zile zinazopewa nafasi ya kutwaa taji (la mwaka huu) la Ligi ya Klabu Bingwa."

Kuhusiana na Ronaldo, Messi alisema: "Hatuchezi ili kuangalia nani ni mkali zaidi kati yetu. Kazi ya kulinganisha ni ya vyombo vya habari."

Mwishowe, alizungumzia timu yake ya taifa ya Argentina na gwiji Diego Maradona: "Nilikuwa na Diego katika timu ya taifa na mambo yalikuwa mazuri. Kama kuna siku ataiongoza Barcelona hilo mimi sijui na haliko kwangu."

Hivi karibuni, Barcelona imejikuta katika wakati mgumu baada ya kupokea kipigo kisichotarajiwa katika mechi yao ya kwanza ya hatua ya 16-bora dhidi ya AC Milan (2-0) na kisha wakachapwa na mahasimu wao Real Madrid mara mbili mfululizo ndani ya siku tano kwa mabao 3-1 na 2-1.

No comments:

Post a Comment