Thursday, March 7, 2013

BARCELONA YAPANIA KUMTWAA NAHODHA WA ARSENAL THOMAS VERMAELEN KWA DAU LA BIL. 38/- ... LENGO NI KUPATA MBADALA WA MABEKI CARLES PUYOL NA ERIC ABIDAL WANAOONEKANA KUKARIBIA MWISHO WA ZAMA

Thomas Vermaelen
BARCELONA, Hispania
KLABU ya Barcelona inayoongoza katika La Liga, Ligi Kuu ya Barcelona, imeanza kumfuatilia kwa karibu nahodha wa Arsenal, Thomas Vermaelen kwa nia ya kumsajili, imefahamika.

Gazeti la The Sun la England limeripoti leo kuwa vigogo hao wa Hispania wanatafuta beki wa kati atakayeendana na staili yao ya kujenga mashambulizi kuanzia kwa mabeki.

Barca wanajua kuwa Carles Puyol, 34, na Eric Abidal, 33, wanaelekea ukingoni mwa nyakati zao za kucheza soka kwa kiwango cha juu.

Vermaelen, 27, anapewa nafasi kubwa kwenye kambi ya Barca na inaaminika kwamba klabu hiyo ya Hispania iko tayari kuweka mezani dau la paundi za England milioni 15 (Sh. bilioni 38) ili kuilainisha Arsenal na kumtwaa beki huyo kisiki.

No comments:

Post a Comment