Sunday, February 3, 2013

ROONEY AIPAISHA MAN UNITED POINTI 10 KILELENI

Gooooooooo!..... Wayne Rooney wa Manchester United akifunga goli lake dhidi ya Fulham wakati wa mechi yao ya Ligi Kuu ya England kwenye Uwanja wa Craven Cottage mjini London, England Februari 2, 2013.

Humu mbona mi napita.... Wayne Rooney wa Manchester United akichana "msitu" wa mabeki wa Fulham wakati wa mechi yao ya Ligi Kuu ya England kwenye Uwanja wa Craven Cottage mjini London, England Februari 2, 2013.

Niliwaambia napita... Wayne Rooney wa Manchester United akipita katika "msitu" wa mabeki wa Fulham wakati wa mechi yao ya Ligi Kuu ya England kwenye Uwanja wa Craven Cottage mjini London, England Februari 2, 2013.
GOLI la 'usiku' kutoka kwa Wayne Rooney ugenini dhini ya Fulham liliisaidia Manchester United kuongeza tofauti ya pointi kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu ya England kufikia pointi 10.

Rooney alikimbia kwenda mbele katika dakika ya 78 na kukutana na mpira mrefu kutokea nyuma uliopigwa na Jonny Evans na kufunga kiufundi kwenye kona ya nyavu na kuandika bao lake la 10 katika mechi 10.

Straika huyo mapema aligongesha nguzo ya goli katika mechi ya wazi ambayo timu zote zilitishia, huku shuti la Bryan Ruiz wa Fulham pia likigonga mwamba.

Kichwa cha Ruiz pia kiliochwa juu ya mstari kabla ya Rooney kufunga la ushindi.

Katika dakika za lala salama zilizojaa ushindi, Fulham walinyimwa goli wakati straika wa Man United, Robin van Persie alipooosha kwenye mstari kichwa Philippe Senderos.

Na huku wenyeji wakipanda mbele kusaka la kusawazisha, Javier Hernandez 'Chicharito' alikimbia peke yake lakini umakini wa kipa Mark Schwarzer uliwanyima Man United goli la pili. 

Matokeo ya mechi zote za jana Jumamosi za Ligi Kuu ya England:

No comments:

Post a Comment