Callejon: Alichofanya Messi si sahihi |
MSHAMBULIAJI wa Real Madrid, Jose Callejon ameelezea alichoshuhudia kuhusiana na tukio baina ya Lionel Messi na Alvaro Arbeloa kwenye maegesho ya magari ya Uwanja wa Bernabeu: "Nadhani kitendo cha Messi kusubiri saa nzima na nusu ili kumvaa mchezaji mwingine si sahihi".
Zaidi, Callejon alisema hiku kuhusiana na majibizano baina ya Muargentina huyo na kocha msaidizi wa Real, Karanka, katika njia ya kuelekea kwenye vyumba vya kuvalia: "Niliona namna ambavyo Messi alimuita Karanka 'kibaraka wa Mourinho kwa sababu nilikuwa nyuma yake."
"Pengine mambo kama haya yakitokea wakati wa mechi ni sawa kwa sababu mambo yanakuwa yamemkaba shingoni na unaweza kuyajutia baadaye, lakini kumfuata mchezaji mwingine mbele ysa mkewe baada ya mechi, hilo si sahihi. Watu wema si wema siku zote, na watu wabaya si wabaya siku zote. Baadhi ya mambo yanapelekwa mbali mno. Nje ya uwanja, wakati mambo yako moto, yanaweza kusemwa yakabaki uwanjani, lakini hayasemwi wakati tukishatulizwa," alisema.
Callejón aliulizwa hadhani kama tukio hilo la Messi linafanana na la kocha wao Jose Mourinho alichofanya kwenye maegesho ya magari ya Nou Camp na alijibu: "Tukio lile lilikuwa tofauti. Mourinho alisubiri kwenye maesho lakini hakusema kitu."
Mshambuliaji huyo pia alizungumzia "Clásico" akisema: "Ilikuwa mechi nzuri sana. Lilipigwa soka la maana, huku timu mbili kubwa zikichuana kisawa sawa, na mambo yalikuwa magumu kwetu. Mambo yalianza kutuwia ugumu, lakini sasa timu yoyote inaweza kufuzu. Kwetu yalikuwa matokeo mazuri."
No comments:
Post a Comment