Monday, February 11, 2013

RONALDO HUENDA AKATUA PSG - WENGER

Cristiano Ronaldo

KOCHA wa Arsenal, Arsene Wenger amesema anamuona nyota wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo akijiunga na PSG siku moja.

Wenger anaamini kwamba PSG wanaandaa ofa nono kwa ajili ya kumhamishia 'supastaa' huyo Ufaransa.

"Huwezi kuondoka Real Madrid kama Real Madrid hawataki uondoke," Wenger aliiambia Telefoot.

"Lakini nina hakika na jambo moja. PSG wanamhitaji Cristiano Ronaldo."

Madai yake yalipata sapoti ya mshambuliaji wa zamani wa timu ya taifa ya Ureno, Pauleta, ambaye alichezea PSG, klabu mpya ya David Beckham, baina ya mwaka 2003 na 2008.

Alisema: "PSG wanao uwezo wa kumnunua na wanaye mkurugenzi wa michezo wa ukweli, Leonardo, ambaye ana upeo, sasa kwanini (wasimnunue)?"

No comments:

Post a Comment