Monday, February 11, 2013

ADEBAYOR KUADHIBIWA TOTTENHAM KWA KUCHELEWA KURUDI

Emmanuel Adebayor

KOCHA wa Tottenham, Andre-Villas Boas amesema klabu hiyo itamuadhibu mshambuliaji Emmanuel Adebayor kwa kuchelewa kurejea kutokea kwenye fainali za Mataifa ya Afrika.

Spurs walilazimika kumtumia ndege binafsi ili kumrejesha mshambuliaji huyo wa timu ya taifa ya Togo mwenye umri wa miaka 28 kwa ajili ya kuwahi mechi waliyoshinda 2-1 Jumamosi dhidi ya Newcastle.

No comments:

Post a Comment