Monday, February 11, 2013

MKATABA MPYA UNAMUINGIZIA MESSI EURO 230,000 BAADA YA KODI KWA WIKI... NI SAWA NA SH. MILIONI 495 KWA WIKI

Lionel Messi akiwa na tuzo ya Ballon d'Or ya Mwanasoka Bora wa Dunia.
Messi siku aliposaini mkataba mpya Barcelona

MKATABA mpya wa nyota wa Barcelona, Lionel Messi unamuingizia euro 230,000 (sawa na Sh. milioni 495) taslimu anazokwenda nazo nyumbani KWA WIKI baada ya makato ya kodi.

Radio Punto Pelota ya Hispania imesema kwamba ukijumlisha na bonasi, mkataba mpya wa Messi ambao utaenda hadi mwaka 2018 utamuingizia euro milioni 12 (sawa na Sh. bilioni 25.8) kwa mwaka.

Majumuisho ya bonasi yanamaanisha ikiwa atashinda tuzo ya Ballon d'Or, atacheza asilimia 60 ya mechi, atashinda Kombe la Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya na ubingwa wa Ligi Kuu ya Hispania.

No comments:

Post a Comment